Kujibu hili kwa ufupi ni kuwa Sidhani kama kuna haja ya kununua iPhone 16 kama unayo iPhone 15 Pro Max..?
Kwa kuwa hili ni pendekezo la mtu ni ngumu sana kutoa jibu la moja kwa moja, lakini nadhani kama wewe ni mmoja ya watu ambao hufikiria zaidi kuhusu teknolojia (Specs and vitu vingine) basi ni muhimu kupata toleo jipya, Lakini kama wewe ni mtumiaji wa kawaida hii ni tofauti kwani ina tegemeana na bajeti yako, nini umependa kwenye simu hiyo, na mambo mengine mengi ambayo ni mapendekezo binafsi.
Ushauri wangu ni kuwa ni vyema kununua toleo la nyuma kama unataka kununua iPhone (Yaani toleo la nyuma ya toleo jipya mfano iPhone 15 Pro Max wakati mwingine hata toleo la nyuma zaidi kwa mfano iPhone 14 Pro Max) au kama ni mtumiaji wa toleo la nyuma iPhone 15 Pro Max basi ni vyema kubaki na simu hiyo angalau kwa mwaka mmoja au zaidi kabla ya kufikiria kubadilisha simu yako.