Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limemtaja mwanafunzi aliyehitimu shule ya msingi St Anne Marie iliyopo mkoani Dar es Salaam, Eluleki Evaristo Haule kuwa ndiye aliyeibuka kinara katika matokeo ya mtihani ya Darasa la Saba 2021.
Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa bora kitaifa ni wale ambao wamepata alama nyingi zaidi kuliko wenzao kwenye masomo sita waliyotahiniwa.
Wanafunzi 10 bora kitaifa matokeo darasa la saba (2021)
- Nafasi ya pili ni Happy Joseph Deus kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mkoa wa Mara
- Nafasi ya tatu ni John Chacha Charles kutoka Twibhoki ya Mara.
- Nafasi ya nne ni Joshua Mahende Jacob kutoka shule ya msingi Twibhoki iliyopo Mara.
- Nafasi ya tano ni Eva Sebastian Chengula kutoka shule ya msingi Fountain of Joy ya Dar es Salaam.
- Nafasi ya sita ni Joctan Samwel Matara kutoka Twibhoki ya Mara.
- Nafasi ya saba ni Barnaba Jumanne Magoto kutoka shule ya msingi Twibhoki ya Mara.
- Nafasi ya nane ni Rahma Ombi Juma kutoka shule ya Mtuki Highland ya Dar es Salaam.
- Nafasi ya tisa ni Juliana John Shimbala kutoka St Joseph’s.
- Nafasi ya kumi ni Jackline Manfredy kutoka shule ya Masaka iliyopo Dar es Salaam.