Kama unataka kutengeneza Mpesa VISA Card kwaajili ya kufanya manununu mbalimbali mtandaoni unaweza kutumia njia mbili kubwa, njia ya kwanza ni kupitia USSD code yaani kwa kupiga * 150 * 00 # au kwa kutumia App ya Mpesa, unaweza kuchagua njia ambayo ni rahisi zaidi kwako.
Jinsi ya Kutengeneza Mpesa VISA Card kwa kutumia USSD Code
- Hatua ya kwanza bofya * 150 * 00 #
- Chagua namba 4 (Lipa kwa Mpesa)
- Chagua namba 6 (Mpesa VISA Card)
- Chagua namba 1 (Tengeneza Kadi)
Baada ya hapo utapokea namba za kadi yako zikiwa pamoja na CVV ambazo zipo idadi ya namba 3 na pia tarehe ya kuisha kwa muda wa kadi yako. Vitu vyote hivyo ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyo tumika kufanya malipo kwenye mitandao mbalimbali.
Jinsi ya Kutengeneza Mpesa VISA Card kwa kutumia Mpesa App
Ili kutengeneza Mpesa VISA Card kwa kutumia app, moja kwa moja pakua app ya Mpesa Tanzania kupitia masoko ya App Store (iOS) na Play Store (Android). Unaweza kupata app hizo kupitia link hapo chini.
Download kwa Android
Click to reveal
Download kwa Android
Click to hide
Download kwa iOS
Click to reveal
Download kwa iOS
Click to hide
Baada ya kupakua na kuinstall app ya Mpesa Tanzania, sasa endelea kwa kujisajili kwa kuingiza namba zako za siri mwanzo kabisa wa app hii. Baada ya hapo utaruhusiwa kuingia ndani ya app hii na moja kwa moja chagua sehemu ya Huduma iliyopo chini kabisa mwisho wa app hiyo, Baada ya hapo utaona kadi ya Mastercard bofya hapo kisha subiri kidogo na utapelekwa kwenye ukurasa wenye maelezo yote ya muhimu.
Kama ni mara yako ya kwanza unatumia sehemu hii bofya sehemu ya Tengenez kadi, moja kwa moja utapokea taarifa za kadi yako kama nilivyo kwambia kwenye maelezo hapo juu.