YouTube channel ni huduma inayotolewa na kampuni ya Google, huduma hii humpa mtu yoyote mwenye umri sahihi uwezo wa kutengeneza channel ambayo anaweza kupakia maudhui moja kwa moja. Kwa hapa Tanzania ni muhimu kuhakikisha unafuata vigezo na masharti ya Mamlaka ya mawasiliano TCRA kabla ya kuamua kufungua channel ya kupakia maudhui mtandaoni.
Kama tayari umefuata vigezo na masharti yote ya kupata leseni kutoka kwa mamlaka husika, moja kwa moja unaweza kutengeneza YouTube channel kwa kufuata hatua hizi chache.
- Tembelea YouTube.com
Hatua ya kwanza tembelea Youtube.com kisha ingia kwa kutumia akaunti yako ya Google. Hadi hatua hii na uhakika tayari unayo akaunti ya Google, kama huna basi hakikisha unatengeneza kwanza akaunti ya Google kabla ya kuendelea.
- Tengeneza YouTube channel kwa kompyuta
Kama unatumia kompyuta moja kwa moja bofya kitufe cha sura ya profile picture yako ndani ya mtandao wa youtube.com kisha chagua sehemu ya Create channel.
Baada ya hapo chagua kati ya kutengeneza channel kwa kutumia jina lako au kwa kutumia jina la biashara, hii ni muhimu kwani utaweza kubadilisha baadae hivyo fanya maamuzi sahihi.
Baada ya hapo chagua jina la channel yako kisha kubali vigezo na masharti na endelea kwa kubofya create
Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kutengeneza channel ya YouTube kwa urahisi na haraka. Unaweza kutengeneza pia akaunti kwa kutumia simu au kwa kubofya link hapo chini.
Tengeneza Channel ya YouTube Hapa
Click to reveal
Tengeneza Channel ya YouTube Hapa
Click to hide