UPDATE November: Ni kweli imekuwa changamoto kuwasiliana na huduma kwa wateja wa Vodacom, lakini unaweza kufuata njia hizi kuweza kuwasiliana nao kwa haraka na bila kusubiri kwa muda mrefu.
Bofya 100 kwenye simu yako kisha piga simu baada ya maelezo, subiri ili kuendelea kwa kiswahili. Baada ya hapo bonyeza mbili 2 kwa matatizo mengine. Baada ya hapo Bonyeza 1 kwa huduma za M-Pesa, Bonyeza moja 1 ambayo ni kusahau PIN yako, Hatua inayo fuata utaulizwa kama namba imesajiliwa na taarifa zako bonyeza 1 kama vingenevyo bonyeza mbili, hapa chagua 1. Kisha moja kwa moja bila kuchelewa simu itapokelewa na mtoa huduma wa Vodacom. Hapa hata kama tatizo halihusiani na PIN utaweza kupata maelekezo.
Kwa ujumla namba ya kuwasiliana na Voda ni kubofya kwa mpangilio namba hizi baada ya kupiga 100. Utabofya 2 1 1 1.
Hope this helps!