Kama kwa namna yoyote ungependa kutuma ujumbe kwa mtu na mara baada ya kusoma ujumbe huo meseji hiyo ijifute basi makala hii ni kwajili yako. Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia fupi na rahisi ambayo unaweza kutumia pale unapokuwa na uhitaji wa hutumia meseji ya mtindo huo.
Kumbuka hadi sasa bado hakuna uwezo wa kufuta SMS ambayo umetuma kwa mtu hivyo njia hii itakusaidia kuweza kutumia njia mbadala ambayo inaweza kukusaidia sana.
Jinsi ya Kutuma SMS inayojifuta Yenyewe
- Ingia kwenye tovuti hii hapa kisha moja kwa moja andika ujumbe waka kwenye sehemu ya kuandika inayo jitokeza kwa juu.
- Baada ya kumaliza kuandika bofya chagua sehemu ya Show Options kisha baada ya hapo kwenye sehemu ya Note self-destructs chagua after reading it. Weka alama ya tiki kwenye chumba chenye maneno Do not ask for confirmation before showing and destroying the note. Kisha kwenye sehemu ya Destruction notification weka barua pepe yako. Baada ya hapo chagua create note.
- Baada ya hapo utaletewa Link maalum ambayo unatakiwa kucopy link hiyo kisha mtumie mtu unaetaka apokee ujumbe unataka ujifute kwa njia ya SMS.
Baada ya hapo pale tu mtu atakapo pokea link hiyo na kuifungua atapelekwa kwenye ujumbe wake na mara baada ya kumaliza kusoma moja kwa moja ujumbe huo utafutika.