Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Whats App Kusitisha Kutoa Huduma kwa Vifaa vya Nokia na Blackberry

Whats App Kusitisha Kutoa Huduma kwa Vifaa vya Nokia na Blackberry Whats App Kusitisha Kutoa Huduma kwa Vifaa vya Nokia na Blackberry

Application ya kisasa ya Whatsapp Kupitia blog yake imetangaza kuacha kutoa huduma yake kwa watumiaji wa baadhi ya vifaa kufikia mwaka 2017, vifaa hivyo ambavyo havitaweza kusupport kutoa huduma ya whatsapp kufikia mwaka 2017 ni Blackberry 10 OS, pamoja na vifaa vingine vyote vinavyotumia OS ya BlackBerry pia Nokia Symbian S40, Symbian S60 na vifaa vinavyotumia Android za zamani kama Android 2.1 Eclair, Android 2.2 Froyo na Window Phone 7.1 OS.

Blog hiyo ya whatsapp iliweka tangazo hilo ilikisema vifaa hivyo havitaweza kutoa huduma ya whatsapp kufikia mwisho wa mwaka huu. Kampuni inayosimamia whatsapp ilisema kipindi ilipo anza kutoa huduma za whatsapp mwaka 2009 soko lilikua tofauti. Kipindi hicho Operation System za Android na iOS zilikua zikitumiaka chini ya asilimia 25% ya vifaa vyote, wakati huo Operation System za Blackberry na Nokia zilikua zinatumiaka kwa asilimia 70% ya vifaa vyote, kwa sasa kuna mabadiliko makubwa sana ya vifaa hivi.

Advertisement

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa “mapoja na vifaa hivyo kuwa na historia kubwa na application ya Whatsapp tunaondoa vifaa hivyo kutokana na kutoku-kidhi mahitaji ya muhimu tunayoitaji ili kukuza application ya Whatsapp kwa siku zijazo” kama ilivyoandikwa kwenye sehemu ya tangazo hilo.

“Huu ni uwamuzi mgumu sana lakini ni uwamuzi wa lazima ili kuendelea kuunganisha ndugu, jamaa na marafiki kwa kutumia application ya whatsapp. Kama unatumia moja kati ya vifaa vinavyotumia Operation System za Blackberry na Nokia tunashauri kubadilisha kifaa chako na kutafuta vifaa vinavyotumia Android iOS au Window Phone kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kuendelea kufurahia huduma hii ya Whatsapp” iliandika blog hiyo.

Wiki iliyopita Whatsapp ilitimiza miaka 7. Kwenye tangazo hilo kampuni hiyo ilitangaza kufikia watumiaji bilioni 1. “Hiyo ni kama kusema katika kila watu saba duniani kuna mtumiaji mmoja anaetumiaWhatsapp kila mwezi” blog hiyo iliandika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use