Tigo Yaungana na Mastercard Kuleta Huduma ya Masterpass QR

Tigo Tanzania Kuanza kupokea husuma za Masterpass QR
Tigo Tanzania Masterpass QR Tigo Tanzania Masterpass QR

Kampuni inayotoa huduma za simu ya Tigo Tanzania hivi karibuni imeungana rasmi na kampuni ya huduma za kifedha ya MasterCard ili kuleta huduma ya Masterpass QR kwa watumiaji wa huduma za kifedha za Tigo Pesa.

Ripoti kutoka tovuti ya Business Chief zinasema, MasterCard imetangaza hayo kupitia mkutano wa MWC 2018 au Mobile World Congress unaofanyika huko nchini Barcelona. MasterCard kupitia kwa msemaji wake imesema kuwa imeamua kuungana na Tigo Tanzania kwa sababu huduma ya Tigo Pesa ni moja kati ya huduma inayo tegemewa sana Hapa Tanzania huku ikiwa na watumiaji zaidi ya milioni 7 ambao watenda kufurahia huduma hiyo.

Advertisement

Masterpass QR ni huduma inayo mruhusu mteja kuweza kulipia bidhaa mbalimbali kwa urahisi kwa kutumia simu ya mkononi kwa kuscan QR code maalum kwa kutumia kamera ya simu ya mkononi na hii uleta urahisi kati ya muuzaji wa bidhaa pamoja na mteja kwa kurahisha njia ya malipo.

Hata hivyo huduma hiyo inategemewa kuwezeshwa kwenye Programu ya Tigo Pesa App ambapo wateja wa Tigo wataweza kulipia bidhaa kwa urahisi kupitia App hiyo. Huduma hii inategemewa kuwezeshwa baadae katikati ya nusu ya mwaka huu 2018. Kujua zaidi kuhusu Masterpass QR tembelea ukurasa huu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use