Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zuia Google Kujua Kuhusu Wewe Kwa Kuzima Settings Hizi

Google Inajua mahali ulipo hata kama umezima location. Zuia google kujua ulipo kwa njia hizi
Zuia Google Kujua Kuhusu Wewe Kwa Kuzima Settings Hizi Zuia Google Kujua Kuhusu Wewe Kwa Kuzima Settings Hizi

Kama wewe ni mtumiaji wa apps mbalimbali za Google basi ni wazi kuwa Google inafahamu mambo mbalimbali kuhusu wewe ikiwa pamoja na sehemu ulipo. Kuliona hili kupitia makala hii nitaenda kuonyesha settings ambazo ni muhimu kuzima kuzuia Google kujua kuhusu wewe.

Kwa mfano kwa kutumia Google Map, Google huendelea kujua mahali ulipo muda wote hata kama umezima sehemu ya location kwenye simu yako. Kwa mujibu wa Google, data hizo zinazo kusanywa hutumika kwaajili ya kufanya apps unazotumika kuwa bora zaidi na data hizo hazishirikishwi na kampuni yoyote au mtu yoyote.

Advertisement

Kama kwa namna yoyote unahitaji kuzima sehemu hizi kabisa basi makala hii ni kwa ajili yako. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Jinsi ya Kuzuia Google Kujua Sehemu Ulipo

Zuia Google Kujua Kuhusu Wewe Kwa Kuzima Settings Hizi

Kama unataka kuzima kabisa njia ya Google kujua mahali ulipo unaweza kutumia njia hii kuweza kuzima kabisa sehemu ya Google’s location tracking ikiwa pamoja na njia za Google kujua unapendelea nini zaidi.

1. Fungua Google.com kwenye simu yako au kompyuta, hakikisha umeingia kwenye akaunti yako.

2. Bofya sehemu ya user icon kisha chagua au unaweza kubofya hapa Manage your Google account.

3. Baada ya hapo bofya sehemu ya Privacy & personalization.

4. Baada ya hapo bofya Things you’ve done and places you’ve been.

5. Bofya sehemu ya Location history ambayo ipo ndani ya box la History settings box. Baada ya hapo bofya Activity Controls.

6. Chini ya sehemu ya Location History, bofya kitufe ambacho kipo kulia ambacho kimeandikwa Turn off. Baada ya kubofya utaona Windows mpya imefunguka.

7. Songea mpaka chini mwisho wa Window husika na bofya Pause.

Kitatokea Nini Baada ya Kuzima Sehemu Hii

Kwa kuzima sehemu hii Google haita weza kujua zaidi sehemu gani ambazo unapendelea zaidi hivyo haitoweza kuonyesha matangazo ambayo yanafanana na sehemu ambazo una zipendelea zaidi. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unapendelea usalama zaidi kuliko kupata huduma unazo zipendelea zaidi basi ni muhimu kuzima sehemu hii.

Jinsi ya Kuzuia Google Kujua Kuhusu Wewe

Zuia Google Kujua Kuhusu Wewe Kwa Kuzima Settings Hizi

Kama unataka kuzuia Google kujua kuhusu wewe, kama vile tovuti ambazo unatembelea zaidi, matangazo ambayo una angalia na mengine mengi basi unaweza kuzima sehemu hii kupitia njia hizi.

1. Fungua Google.com kwenye simu yako au kompyuta, hakikisha umeingia kwenye akaunti yako.

2. Bofya sehemu ya user icon kisha chagua Manage your Google account au unaweza kubofya hapa Manage your Google account.

3. Baada ya hapo bofya sehemu ya Privacy & personalization.

4. Baada ya hapo bofya Things you’ve done and places you’ve been.

5. Baada ya hapo chagua Web & App Activity.

6. Chini ya sehemu ya Web & App Activity, bofya kitufe ambacho kipo kulia ambacho kimeandikwa Turn off. Baada ya kubofya utaona Windows mpya imefunguka.

7. Songea mpaka chini mwisho wa Window husika na bofya Pause.

Kitatokea Nini Baada ya Kuzima Sehemu Hii

Kwa kuzima sehemu hii Google haita weza kujua historia ya tovuti ulizo tembelea, apps ambazo unatumia kwa wingi ikiwa pamoja na maneno ambayo umetafuta kupitia kwenye Google. Hii itazuia google kuonyesha matangazo yanayo fanana na mambo unayo fanya mtandaoni.

Hitimisho

Kwa kufanya hatua hizi utaweza kuzuia Google kujua zaidi kuhusu wewe, sehemu ambazo umefikiwa na mambo mengine mbalimbali. Kumbuka kuwa baada ya kuzima sehemu hizi unaweza kuona mabadiliko wakati unatumia huduma na apps za Google.

Mbali na hayo kumbuka kuwa Google inaweza kuendelea kuhifadhi data zako za awali na unaweza kufuta data zako kwa kutembelea ukurasa huu. Kumbuka hakikisha umeingia kwenye akaunti yako ya Google.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use