Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Kupitia njia hii utaweza kusaidia bando kudumu kwa muda mrefu unapo angaia video YouTube
Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Ni wazi kuwa YouTube ni mmoja ya mtandao maarufu wa kuangalia video za kuelimisha, kuburushi na kufurahisha. Lakini pia kutokana na gharama za vifurushi ni rahisi sana kuishiwa bando kwa haraka pale unapo angalia video kupitia YouTube App.

Kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi ambayo inaweza kusaidia sana kuweza kupunguza matumizi makubwa ya data hasa pale unapo angalia video za YouTube kupitia app ya YouTube kwenye simu yako. Njia hii ni bora na inaweza kufanya kazi kwenye simu zote za Android pamoja na iOS.

Advertisement

YouTube  Android App

Kwa kuanza moja kwa moja fungua app ya YouTube kisha bofya kwenye picha yako ya profile ambayo huwa upande wa kulia juu.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

 

Baada ya kubofya hapo, moja kwa moja bofya sehemu ya Settings ambayo inapatikana juu upande wa kulia.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Baada ya kufungua ukurasa wa settings, shuka chini kidogo kisha bofya sehemu ya ‘Video Quality Preferences’ ambayo inapatikana chini kidogo, option ya 9 kutoka chini.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Baada ya kubofya sehemu hiyo utaona sehemu ya kubadilisha quality za video yaani sehemu ya WiFi na Mobile Network.

Kama unatumia data kupita simu yako moja kwa moja Sehemu hii itakusaidia kupunguza Quality ya video pale unapo angalia kwenye simu ili isichukue bando zaidi. Sasa ili kuhakikisha app ya YouTube haichukui bando zaidi unapo tazama video chagua sehemu ya Data Saver.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

YouTube App iOS

Kwa Watumiaji wa iOS hatua zinafanana isipokuwa hatua moja, hakikisha unafuta hatua hizi kuweza kuwasha sehemu hii kupitia iOS.

Fungua app ya YouTube ya iOS kisha bofya sehemu ya Profile au “You” inayopatikana chini upande wa kulia.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Kisha baada ya hapo bofya sehemu ya Settings iliyopo juu upande wa kulia, alama ya kipuli cha mashine.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Baada ya hapo kwenye ukurasa wa Settings tafuta sehemu ya Video quality preference, sehemu hii inapatikana chini kidogo ya ukurasa huo.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Kisha chagua sehemu ya On Mobile Network kama unatumia bando ya simu yako moja kwa moja, ila chagua Wi-Fi kama unatumia Wi-Fi au Hotspot. Kwa mfano huu tutachagua Mobile Network.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Kisha baada ya kufungua ukurasa huu sasa chagua sehemu ya Data Saver ambayo ni inapatikana juu kwenye sehemu ya Mobile Networks.

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube

Hakikisha sehemu hii ya kwanza ya Video Quality on Mobile ndio inakuwa kwenye Data Saver, Sehemu hii itasaidia kuwa wakati una angalia video data haito tumika kwa wingi kwenye simu yako na hivyo utaweza kuangalia video kwa haraka lakini haito tumia data kwa wingi.

Pia ni vyema kukumbuka kuwa sehemu hii hupunguza Quality ya video mara nyingi kwenye simu huwezi kuona tofauti mara moja, lakini kwenye vifaa vyenye screen au kioo kikubwa unaweza kuona tofauti ya Quality.

Kama unahitaji kuona video ikiwa angavu sana unaweza kuzima sehemu hii na kuchagua sehemu ya Auto au Higher picture quality ambayo uchukua data zaidi.

Bila shaka hadi hapo umeweza kupunguza matumizi ya data pele unapo angalia video kupitia YouTube App, kumbuka njia hizi ni sawa kwa watumiaji wote wa Android pamoja na iOS. Kama unataka kujifunza mengi kwa vitendo unaweza kujiunga nasi kuptia channel yetu ya YouTube Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use