Kuanzisha biashara kunahitaji umakini pamoja na kujituma ndio maana hivi karibuni kampuni ya ZoomTanzania kupitia tovuti yake ya zoomtanzania.net imeonekana kuwa na yote hayo baada ya kushinda tuzo ya tovuti bora kwa mwaka 2016, hii ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa kampuni hiyo kushinda tuzo hiyo baada ya kushinda tena tuzo hiyo mwaka 2015.
Katika tuzo hizo za Tanzania Leadership Awards zilizotolewa na kuandaliwa na kampuni ya Purple Cow Media Limited zoomtanzania ilipata tuzo hiyo pamoja na makampuni mengine yalio onekana kuleta mabadiliko pamoja na kufanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali hapa Tanzania. Hii ndio list ya washindi hao kama ilivyo andikwa na mtandao wa zoomtanzania.
- Category: Best place to work
Winner: Smart Codes - Category: Innovative company of the year
Winner: E-Fm Radio - Category: Domestic airline of the year award
Winner: Coastal Aviation - Category: NGO of the year
Winner: GSM Foundation - Category: Telecom company of the year
Winner: Tigo Tanzania - Category: Restaurant of the year
Winner: Cape Town Fish Market. - Category: Hotel of the year
Winner: Hyatt Regency Hotel - Supermarket of the year
Winner: Food Lovers Market - Category: TV Channel of the Year
Winner: Azam TV - Category: Website of the year
Winner: ZoomTanzania
Tuzo hizo za Tanzania Leadership Awards zilifanyika siku ya ijumaa ya tarehe 27 mwezi January mwaka huu 2017 kwenye hoteli ya Hyatt Regency Hotel hapa Dar es salaam, Tanzania.
Kuwa wakwanza kupata habari za teknolojia kwa kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na channel yetu ya youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya Video.