Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu TV Bora Zenye Programu ya Android Kutoka Sony

Angalia Mapitio ya TV hiyo yenye Kutumia OS ya Android
Android TV Android TV

Kwa sasa kuna tv nyingi sana ambazo zinakuja na programu mbalimbali ndani yake tv hizi zinafaamika kwa jina maarufu la (Smart Tv), tofauti kabisa na tv nyingine hizi zinakuwa na uwezo wa kufanya mambo mengine mengi kama vile kuperuzi kwenye mtandao, kushusha programu mbalimbali kutoka kwenye mitandao pamoja na mambo mengine mengi.

Advertisement

Hata hivyo kampuni nyingi maarufu duniani zimejikita katika utengenezaji wa tv za aina hii (Smart Tv) moja kati ya kampuni hizo ni kampuni maarufu ya Sony, kampuni hii inajulikana sana kwa utengenezaji wa tv bora kama vile Sony KD-75X9405C pamoja na zingine nyingi ambazo kwa sasa ndio tv bora kabisa. Hadi kufikia mwaka 2015 kampuni hiyo ya sony yenye makazi yake huko Minato, Tokyo katika nchi Japan ilianza kujikita rasmi katika utengenezaji wa tv zenye uwezo wa kutumia programu maalum ya Android, kwa kushirikiana na kampuni nyingine maarufu duniani kama Google Sony iliweza kutengeneza Tv zake hizo ambazo zilikua zikitumia programu hiyo inayofanya tv yako iwe janja na bora zaidi.

Tv hizo zenye jina la Android Tv Sony BRAVIA zinauwezo wa kushusha programu mbalimbali za Android kutoka katika Play Store yaani kama ilivyo simu yako ya mkononi ya android, tv hii inakuwezesha pia kuangali programu mbalimbali kutoka katika mtandao moja kwa moja kwenye tv yako. Hata hivyo kuna watu wengi sana wananunua tv hasa hapa Tanzania bila kujua kuwa Tv zao zinauwezo wa android, ili kujua kama tv yako ya Sony inatumia programu maalumu ya android bofya kitufe maalumu kilicho andikwa “Home” na utaanza kutumia programu hiyo moja kwa moja bila tatizo.

Kwa wale ambao tv zao hazina programu hii maalumu ya android unaweza uka nunua kifaa maalumu cha “Android Tv Box” kifaa hichi kitakuwezesha kutumia programu ya android moja kwa moja kwenye Tv yako ya kawaida pia utakua na uwezo wa kushusha programu maalumu kwenye simu yako ambayo itabadili simu yako kuwa (remote) ambapo utaweza kuendesha tv yako kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kifaa hicho huunza kuanzia dollar za kimarekani $150 mpaka $99.99 kwenye mtandao wa Amazon.Zifahamu TV Bora Zenye Programu ya Android Kutoka Sony

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use