Kampuni ya Google kupitia mtandao wake wa kijamii wa YouTube imetangaza kupitia blog yake kuwa sasa kuna aina mpya ya matangazo ambayo yatakua yakitokea kama video fupi ya sekunde 6, habari hizo zilizo andikwa na meneja wa bidhaa hapo YouTube Mr Zach Lupei zinasema matangazo hayo ni sehemu ya mpango kazi wa kuboresha mtandao huo maarufu kwa kushare video wa YouTube.
Hata hivyo blog hiyo iliendelea kuandika kuwa watumiaji wa mtandao huo hawatakua na uwezo wa kusogeza (SKIP) matangazo hayo kwani yanatokea kwa muda mfupi sana hivyo kutakua hakuna haja ya kuyasogeza (SKIP) matangazo hayo iliandika sehemu ya habari kwenye blog hiyo. Hata hivyo hii ni habari njema kwa wale wanaoonyesha matangazo kwenye channel zao kwani hii inamaanisha kuongezeka kwa mapato kutokana na matagazo hayo mafupi maarufu kama “Bumper Ads“.