Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Yaja na Sehemu Mpya ya “Inspiration Tab”

Sehemu mpya ya inspiration itakusaidia kupata idea mpya za video kwaajili ya channel yako
YouTube Yaja na Sehemu Mpya ya "Inspiration Tab" YouTube Yaja na Sehemu Mpya ya "Inspiration Tab"

Mtandao wa YouTube unendelea kufanya mabadiliko mbalimbali na kuelekea mwaka 2025, YouTube inategemea kuongeza vipengele vipya ikiwa pamoja na sehemu nyingi zinazotumia mfumo wa AI au akili bandia.

Kwa kuanza, YouTube hivi karibuni imetangaza ujio wa sehemu mpya ya “Inspiration Tab” ambayo itakusaidia wewe kama mtengenezaji wa maudhui ya video kuweza kupata mawazo ya video gani utengeneze ili kupata wafuasi zaidi.

Advertisement

Sehemu hii mpya ya inspiration TAB ni tofauti kidogo na sehemu ya inspiration inayo patika kupitia YouTube Analytics. Utafuti mkubwa ulipo ni kuwa sehemu hii mpya inakupa uwezo wa kupata mawazo mbalimbali ambayo yana tengenezwa na mfumo wa IA.

YouTube Yaja na Sehemu Mpya ya "Inspiration Tab"

Sehemu hii itakupa mawazo ya Video gani utengeneze na mfumo ambao pengine ni bora kwa kutengeneza video hiyo ikiwa pamoja na hatua za kufuata.

Mbali na hayo sehemu hiyo pia inaweza kukusaidia kutengeneza picha za kuweka kwenye Video zako “Thumbnails” ikiwa pamoja na kupata kichwa bora cha habari kuhusu video yako.

Kupata sehemu hii ingia kwenye akaunti yako ya YouTube, kisha bofya sehemu ya Content kisha utaona sehemu mpya ya “inspiration”. Bofya sehemu hiyo na subiri kidogo kisha otaona baadhi ya mawazo ya video gani utengeneze, mawazo ambayo yame tengenezwa na AI.

Sehemu hii mpya inapatikana kwa watumiaji wa YouTube wenye channel ambazo zipo active, kama bado ujaona sehemu hii kwenye channel yako endelea kusubiri na pengine ndani ya siku zijazo unaweza kuona sehemu moja kwa moja kupitia YouTube Studio.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kutengeneza Video bora za YouTube kwa urahisi na haraka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use