Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Kuja na Aina Mpya za Username (Handle)

Sasa Username ya Youtube itaweza kufanana na TikTok na Twitter
YouTube Kuja na Aina Mpya za Username (Handle) YouTube Kuja na Aina Mpya za Username (Handle)

Mtandao wa YouTube hivi karibuni umetangaza kuwa unakuja na aina mpya ya username ambayo itasaidia watu kupatikana kwa urahisi kupitia mtanda huo.

Aina hiyo mpya ya Username itakuwa tofauti kabisa na username ya awali ambayo ilikuwa ikitumiwa na watumiaji mbalimbali. Kwa mujibu wa YouTube sasa username mpya ya channel itakuwa kama username ya Twitter au mtandao wa Tiktok.

Advertisement

Kwa upande wa channel ya Tanzania Tech sasa utaweza kuona inapatika kwenye kutumia Username hiyo hapo chini.

Youtube.com/@tanzaniatech

Kama unavyoweza kuona sasa username au handle hizo zinakuja na alama ya @ katikati na zitaweza kuonekana hivyo kupitia sehemu ya Stories, kwenye comment, community tab na sehemu mbalimbali kwenye mtandao wa YouTube.

YouTube Kuja na Aina Mpya za Username (Handle)

Pia YouTube imetangaza kuondoa kikwazo cha subscribers 100 na sasa watu wote wataweza kuchagua username yoyote mara tu wanapotengeneza channel. Pia utaweza kubadilisha username hiyo muda wowote.

Mbali na hayo, YouTube imetangaza kuwa kwa channel ambazo tayari zilisha chagua URL hapo awali link hiyo itaendelea kutumia lakini itaonekana kama username yenye handle. Pia unaweza kubadilisha link hiyo muda wowote.

Hata hivyo link zote za zamani zitaendelea kufanya kazi kama kawaida. Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea ukurasa huu kupata taarifa zaidi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use