Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Kuanza Kuficha Idadi ya Subscriber Kwenye Channel Zote

Hutoweza kuona idadi kamili ya subscriber kwenye channel zenye subscribe zaidi ya 1000
YouTube Kuanza Kuficha Idadi ya Subscriber Kwenye Channel Zote YouTube Kuanza Kuficha Idadi ya Subscriber Kwenye Channel Zote

Mtandao wa YouTube unakuja na mabadiliko mapya ambayo yatakuja kwa watumiaji wote wa mtandao huo, mabadiliko hayo yanahusisha zaidi upande wa namba za subscriber ambazo mara nyingi huonekana kama njia ya kujua channel bora kwenye mtandao huo.

Sasa habari mpya hivi karibuni zinasema kuwa, YouTube imetangaza kuanzia mwezi wa nane mwaka huu 2019 itakuwa na mabadiliko mapya ambapo sasa namba hizo zinazoonyesha idadi ya subscriber zitabadilishwa na kufupishwa.

Advertisement

Kwa mujibu wa blog ya YouTube, YouTube imetangaza hatua hiyo huku ikitoa maelezo kuwa, mwanzo namba za subscriber zilikuwa zikisomeka kamili kwa mfano 12,334,455 lakini sasa namba hizo zitafupishwa na kuwa mfano 12,334,455 itakuwa 12 Million. Hata hivyo namba hiyo haitoweza kubadilika mpaka hapo channel husika itakapo fikia hatua nyingine, kwa mfano 12 Milioni haito badilika hadi hapo itakapo fikia 13 Milioni.

YouTube Kuanza Kuficha Idadi ya Subscriber Kwenye Channel Zote

Hata hivyo kwa watumiaji wa mtandao huo wenye channel zenye subscriber chini ya 1000, namba hizo zitaendelea kuonekana kama kawaida hadi hapo channel hizo zitakapo fikisha subscriber zaidi ya 1000. Yani kwa mfano channel ikiwa na Subscriber 2000 basi namba hizo zitaonekana 2k.

Kupitia blog yake Youtube imesema kuwa sehemu hiyo haito athiri idadi kamili ya subscriber, kwani idadi hiyo itaendelea kuonekana kupitia YouTube Analytics ndani ya channel husika. Kwa maneno mengine ni sawa na kusema, mwenye channel pekee ndiye atakaye weza kuona idadi kamili ya subscriber kwenye channel yake mara baada ya channel hiyo kufikisha subscriber zaidi ya 1000.

Mbali na YouTube, Instagram nayo hadi sasa ipo kwenye majaribio ya kufisha idadi kamili ya Likes kwenye picha, huku pia ikifanya majaribio ya muonekano mpya wa profile ili kuangalia zaidi watumiaji wa akaunti husika na sio idadi ya followers.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use