Hivi leo mtandao wa YouTube umetangaza kuwezesha sehemu mpya ambayo itakuwa maalumu kwa kuwasaidia watu wanaotaka kurekodi video mubashara au Live Streaming kuweza kufanya hivyo kwa urahisi kupitia kompyuta zao
Sehemu hiyo ambayo inapatikana kwa kutumia kisakuzi Browser ya Chrome itakusaidia kwenda live kwa kutumia kamera ya kompyuta yako bila kuongeza programu yoyote ile. Kwa sasa sehemu hiyo inapatika kwa kutembelea tovuti ya Youtube kwenye kompyuta kwa kutumia Google Chrome kisha utaona kitufe kipya upande wa kulia juu, bofya hapo kisha bofya Go Live.
Google kupitia mtandao wake imesema kuwa kwa sasa sehemu hiyo inapatikana kwenye mtandao huo kwa kutumia kompyuta pekee, lakini imesema siku za karibuni inatarajia kuwezesha sehemu hiyo kwenye simu za mkononi na kwa kuanza simu zitakazo weza kufanya kazi kupitia sehemu hiyo zitakuwa ni simu za Asus, LG, Motorola, Nokia, pamoja na Samsung.
Kwa sasa sehemu hiyo inapatikana kwa watumiaji wote duniani na inafanya kazi kama unatumia kisakuzi au Browser ya Google Chrome pekee, hivyo kabla ya kujaribu sehemu hiyo hakikisha unatumia kisakuzi hicho cha Chrome kwenye kompyuta yako kisha unaweza kubofya link hii youtube.com/webcam na utanza kurekodi video za mubashara moja kwa moja.