Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Kuja na “Reels” Sehemu ya Stories Kwaajili ya YouTube

Sasa Mtandao wa Youtube nao umekuja na sehemu ya “Youtube Stories”
youtube Reels youtube Reels

Katika harakati za kufanya mtandao wa Youtube kuwa bora zaidi, hivi karibuni mtandao huo utakuwa na maboresho mapya pamoja na aina mpya kabisa za kutumia mtandao huo. Maboresho hayo ambayo sasa yapo kwenye hatua za awali ni pamoja na sehemu inayoitwa “Reels”.

Reels ni sehemu ya Stories kama ilivyo kwenye mitandao ya Snapchat, Facebook na Instagram lakini sehemu hii kwa upande wa mtandao wa Youtube itakuwa na utofauti mkubwa sana.

Advertisement

Sehemu hii itakuja ndani ya kipengele cha “Community”. Kama ulikua hujui kuhusu kipengele hichi hii ni sababu kuwa siku za nyuma kipengele hichi kilikua kinawekwa kwa baadhi ya channel maarufu tu, lakini hadi kufikia siku ya jana Youtube imetangaza kuwa sasa kipengele hicho kitakuwa kwenye channel zote zilizofikisha idadi ya Subscriber elfu kumi (10k) na kuendelea.

Utofauti uliopo ni kuwa Youtube itakupa uwezo wa kuweka video pamoja na kuweka (filter na Sticker) mbalimbali, lakini video zako zitaweza kukaa zaidi ya masaa 24. Mbali na hayo mtumiaji pia ataweza kuweka link za video mbalimbali ndani ya Stories.

Kwa sasa sehemu hii ya Reels iko kwenye hatua za majaribio kwa watu wachache na inategemewa kuwa sehemu hii itakuja hivi karibuni kupitia Application yako ya Youtube ya mifumo yote ya Android na iOS, bado haija julikana kama sehemu hii itakuja pia kwenye tovuti ya Youtube kwa watumiaji wa kompyuta.

Je wewe unaonaje nini maoni yako kuhusu sehemu hii mpya ya Reels.? tuambie kwenye maoni hapo chini. Usasahau kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari za teknolojia kwa haraka zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use