YouTube Kuanza Kuficha Idadi ya Dislikes Kwenye Video Zote

Mtu ambaye sio mmiliki wa channel hatoweza kuona idadi ya dislikes
YouTube Kuanza Kuficha Idadi ya Dislikes Kwenye Video Zote YouTube Kuanza Kuficha Idadi ya Dislikes Kwenye Video Zote

Habari mpya kutoka YouTube, hivi leo YouTube imetangaza kuwa inategemea kuanza kuficha idadi ya dislikes kwenye video zote kupitia mtandao wa YouTube.

Hatua hii inakuja baada ya YouTube kufanya majaribio na kuona kuwa kuondoa idadi ya dislike kwenye video kuna punguza kiasi cha mashambulizi (dislike attacks) ambayo hutokea kwa wabunifu mbalimbali baada ya video zao kupewa dislikes nyingi bila sababu ya muhimu.

Advertisement

Hata hivyo, YouTube imetangaza kuwa kitufe cha dislike kitaendelea kuonekana kama kawaida kwenye video zote na pia mtu ataweza kuendelea ku-dislike video yoyote, lakini idadi ya dislikes hizo haito onekana kama awali.

Mbali na hayo, mmiliki wa channel husika pekee ndio atakuwa na uwezo wa kuona idadi ya dislikes hizo moja kwa moja kupitia YouTube Studio kwenye kipengele cha Analytics.

Hadi sasa video inayo ongeza kwa kuwa na dislikes nyingi kwenye mtandao mzima wa YouTube ni video ya YouTube’s Rewind ya mwaka 2018, ambayo hadi sasa ina takribani dislikes Milioni 19.

YouTube Kuanza Kuficha Idadi ya Dislikes Kwenye Video Zote

Kwa sasa bado YouTube haija tangaza rasmi tarehe halisi ya lini dislikes zitaondolewa kwenye video zote, lakini tegemea kuona mabadiliko hayo siku za karibu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use