YouTube Yaleta Sehemu ya Incognito Mode Kwenye Android

Sasa weka sehemu ya Incognito mode kupitia Android App
YouTube-incognito mode YouTube-incognito mode

Inawezekana umewahi kusikia sehemu ya Incognito mode, lakini kwa namna moja ama nyingine inawezekana ujawahi kuitumia kutokana na kutokuona umuhimu wake. Sehemu hii ni maarufu kwenye browser mbalimbali kama vile Google Chrome, Firefox na nyingine kama hizo.

Matumizi ya sehemu hii mara nyingi ni kwaajili ya kuzima historia za matumizi yako kwenye kivinjari unacho tumia, hii huwa na faida kama unataka kutembelea tovuti fulani lakini hutaki data mbalimbali za kwenye tovuti hiyo zihifadhiwe kwenye kifaa unachotumia.

Advertisement

Sasa kama wote tunavyojua, YouTube ni tovuti namba mbili duniani ambayo hutumiwa na watu wengi duniani kutafuta mambo mbalimbali. Vilevile ni vyema kujua kuwa, mambo mengi unayotafuta kupitia mtandao wa youtube huifadhiwa kwenye historia ya akaunti yako ya Gmail na pia Google hutumia historia hiyo kuweza kuleta video ambazo zinaweza kukuvutia zaidi.

Sasa tukirudi kwenye sehemu mpya ya Incognito Mode kwenye mtandao wa Youtube, sehemu hii itakusaidia kuweza kutafuta video au kutumia mtandao wa YouTube kwa siri bila YouTube kuhifadhi historia ya video ulizo tafuta na kuangalia.

Sehemu hiyo mpya ya Incognito Mode inapatikana kupitia App ya YouTube ya Android na unaweza kiuwasha sehemu hiyo moja kwa moja kwa kubofya sehemu ya profile yako.Kama bado ujapata sehemu hii unaweza kusasisha (update) toleo jipya la App ya YouTube kupitia soko la Play Store.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use