Youtube imetangaza kuanza kutoa huduma ya kuonyesha video za nyuzi 360 lakini kumbuka video zitakazo weza kuonyeshwa kwa teknolojia hiyo ya nyuzi 360 ni zile za moja kwa moja ama kwa jina lingine “Live Streaming” , Pia kampuni hiyo imetangaza kuzindua huduma nyingine ya sauti ijulikanayo kama “spatial audio” teknolojia hii ina saidia kuimarisha sauti hasa ya video au audio zinazo rekodiwa moja kwa moja au Live.
Hata hivyo tayari watu wameshaanza kuonyesha matamasha mbalimbali kwa kutumia teknolojia hiyo mpya ambayo hata ukiwa na smartphone yako ya galaxy S7 pamoja na Gear 360 tu unaweza kurekodi video hiyo ya nyuzi 360. Kumbuka ili kuweza kutengeneza video ya nyuzi 360 ni lazima uwe na kifaa chenye teknolojia hiyo ya 360 lakini katika upande wa kuangalia video hizo huna haja ya kuwa na kifaa cha ziada unaweza kutumia vifaa vya kawaida tu kama kompyuta ama Simu yako ya mkononi.
Tizama mfano wa video hiyo hapo juu kisha bofya vitufe vilivyoko juu upande wa kushoto kuagalia nyuzi 360.