Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Channel 10 Bora kwa Tanzania Mwaka (2019)

Channel hizi 10 zina idadi kubwa ya subscriber kuliko channel zote Tanzania
YouTube Channel 10 Bora kwa Tanzania Mwaka (2019) YouTube Channel 10 Bora kwa Tanzania Mwaka (2019)

Wakati ikikaribia mwisho wa mwaka 2019, hapa Tanzania Tech huwa na taratibu ya kurudi nyuma na kuangalia yote tulio yapitia kwa mwaka mzima. Kwa siku ya leo tunaenda kuangalia channel 10 bora za YouTube kwa hapa Tanzania kwa mwaka 2019.

Kumbuka channel hizi zimepatikana kuwa bora kutokana na kuwa na subscribers wengi kuliko channel nyingine kwa hapa Tanzania. Kama ilivyokuwa kwenye list ya mwaka 2018, list hii imewezeshwa na data kutoka kwenye tovuti ya Socialblade. Pia kumbuka inawezekana idadi ya subscriber iliyotajwa kwenye list hii ikiwa imeongezeka kulingana na muda utakao soma makala hii.

Advertisement

10. MBOSSO

  • Subscriber 712K – Hadi Tarehe 9-12-2019
  • Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018  !new

Mbosso ni msanii wa kimataifa wa muziki wa bongo flava kutoka hapa Tanzania na ni mmoja wa wasanii walio sajiliwa chini ya kampuni ya Wasafi ambayo inaongozwa na Msanii Diamond Platnumz. Channel hii imeanzishwa mwaka 2016 na ina idadi ya video 402 hadi kufikia siku ya leo.

9. AZAM TV

  • Subscriber 759K – Hadi Tarehe 9-12-2019
  • Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018  !new

Azam TV ni channel ya chombo cha habari cha Azam TV Tanzania, channel hii inakupa habari na makala mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa lugha ya kiswahili. Channel hii ni sehemu ya vituo mbalimbali vya habari kutoka kampuni ya Bakhresa Group.

8. BINGO ONLINE TZ

  • Subscriber 768K – Hadi Tarehe 9-12-2019
  • Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018  !new

Bingo Online TZ ni channel ya hapa Tanzania ambayo inakuletea habari mbalimbali za wasanii na udaku kutoka Tanzania, Channel hii ni maarufu zaidi kwa matukio ya Live pamoja na udaku pamoja na matukio ya kila siku. Channel hii imeanzishwa mwaka 2017 na ina idadi ya zaidi ya video 3000 hadi kufikia leo.

7. JAMVI ONLINE TV

  • Subscriber 922K – Hadi Tarehe 9-12-2019
  • Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018  !new

Jamvi TV ni channel ya matukio mbalimbali kutoka Tanzania, channel hii inakuapa habari na makala mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika na Tanzania kwa ujumla. Channel hii imeanzishwa mwaka 2012 na ina idadi ya video 2,058 hadi kufikia siku ya leo.

6. WASAFI MEDIA

  • Subscriber 1.01M – Hadi Tarehe 09-12-2019
  • Channel hii Haikwepo kwenye List ya Mwaka 2018  !new

Wasafi Media ni sehemu ya chombo cha habari cha msanii na mfanyabiashara Nasibu Abdul au Diamond Platnumz, channel hii inaweka video za makala mbalimbali za habari, mchezo, burudani, vichekesho pamoja na mambo mengine mengi. Channel hii imeanzishwa mwaka 2018 na ina idadi ya video 2,937 hadi kufikia siku ya leo.

5. RAYVANNY

  • Subscriber 1.22M – Hadi Tarehe 09-12-2019
  • Channel hii Imepanda ilikuwa namba 6 mwaka 2018  ^imepanda

Rayvanny ni msanii wa kimataifa wa muziki wa bongo flava kutoka hapa Tanzania na ni mmoja wa wasanii walio sajiliwa chini ya kampuni ya Wasafi ambayo inaongozwa na Msanii Diamond Platnumz. Channel hii imeanzishwa mwaka 2016 na ina idadi ya video 460 hadi kufikia siku ya leo.

4. HARMONIZE

  • Subscriber 1.35M – Hadi Tarehe 9-12-2019
  • Channel Hii ilikuwa namba 4 mwaka 2018  =Sawasawa

Harmonize ni msanii bongo fleva wa kimataifa na pia ni mmoja wa wasanii waliokuwa chini ya lebo ya Wasafi ambayo inaongozwa na Diamond Platnumz. Channel hii ilianzishwa mwaka 2015 na kuanzia kipindi hicho hadi sasa ina idadi ya jumla ya video 329 hadi kufikia siku ya leo.

3. GLOBAL TV

  • Subscriber 1.98M – Hadi Tarehe 9-12-2019
  • Channel hii ilikuwa namba 3 mwaka 2018 =Sawasawa

Global TV au Global TV Online ni Channel inayokupa habari mbalimbali za kila siku kutoka ndani na nje ya nchini. Channel hii ilianzishwa mwaka 2011 na ni moja kati ya sehemu ya huduma zinazotolewa na Global Publisher, channel hii ina idadi ya video 26,536 hadi kufikia siku ya leo.

2. MILLARD AYO

  • Subscriber 2.34M – Hadi Tarehe 9-12-2019
  • Channel hii ilikuwa namba 2 mwaka 2018 =Sawasawa

Millard Ayo ni mmoja wa watangazaji maarufu wa kituo cha Clouds Media Group, kupitia channel yake hii utaweza kupata habari mbalimbali za kutoka ndani na nje ya nchi kila siku. Channel ya Millard ayo ilianzishwa mwaka 2012 na kwa muda wote hadi sasa channel hiyo ina idadi ya video 21,947 hadi kufikia siku ya leo.

1. DIAMOND PLATNUMZ

  • Subscriber 2.75M – Hadi Tarehe 9-12-2019
  • Channel hii ilikuwa namba 1 mwaka 2018 =Sawasawa

Channel ya kwanza maarufu zaidi kwa hapa nchini Tanzania ni channel ya mwana muziki wa kimataifa na msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz. Channel yake iliyoanzishwa mwaka 2011 ina idadi ya video 609 hadi kufikia siku ya leo.

Na hizo ndio YouTube channel 10 bora kwa hapa Tanzania, kama unataka kujua channel bora duniani hadi sasa unaweza kusoma hapa kujua channel 10 bora zenye subscriber wengi kuliko channel zote kwenye mtandao wa YouTube.

Kuhakikisha na sisi tunaingie kwenye list hii, endelea kuonyesha support yako kwa ku-subscriber kwenye channel yetu kupitia hapa, Tunashukuru sana kwa Support yako.?

1 comments
  1. Ni njia ipi ambayo hutumika kupokea sasa malipo YouTube kwa kazi unazoweka YouTube?
    Na jins gani kuiweka.?
    Maana kuna mtu ana channel lakini haipokei kitu ?
    Wanakutumiaje?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use