Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Android na iOS Kuja na Sehemu Mpya ya Dark Theme

Sehemu hii ya Dark Theme itakusaidia kulinda macho yako hasa wakati wa usiku
Dark Theme Youtube Dark Theme Youtube

Mtandao wa YouTube hivi leo umeanza kutoa toleo jipya la programu zake zenye maboresho mapya pamoja na ujio wa sehemu ya Dark Theme. Sehemu hii itasaidia kuweka weusi ambao utakuwa unazuia kuumia kwa macho hasa wakati wa usiku.

Sehemu hii ya Dark Theme mwanzoni ilikua kwa watumiaji wa kompyuta pekee ambapo unaweza kuweka muonekano huo mweusi kwa kubofya sehemu ya picha ya ukurasa wako wa Youtube inayopatikana juu upande wa kulia, kisha chagua sehemu ya Dark Theme na utaweza kuweka au kuwasha muonekano huo moja kwa moja.

Advertisement

Kwa upande wa simu, Siku ya leo kumeanza kutoka toleo jipya la programu ya YouTube kwa watumiaji wa iOS ambapo sehemu hiyo itakuwa kwenye sehemu ya Settings inayo patikana kwenye ukurasa wako (profile) ya YouTube.

Kwa watumiaji wa mfumo wa Android sehemu hii inategemewa kuja kwenye mfumo huu kwenye siku za karibuni. Sehemu hii ni muhimu sana kwa afya ya macho yako hasa kama unatumia mtandao wa YouTube wakati wa usiku, kwani mwanga mweupe unao tolewa na vifaa vya kidigital hasa unapo tumia wakati wa usiku huweza kusababisha matatizo makubwa ya macho pamoja na matatizo mengine ya kukosa usingizi na mengine kama hayo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use