Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Yaliyojiri Kwenye Tamasha la Uzinduzi wa Apple iPhone 7

Haya ndio yote yaliojiri kwenye uzinduzi wa simu mpya kutoka Apple iPhone 7
yaliyojiri-jana-kwenye-mkutano-wa-apple yaliyojiri-jana-kwenye-mkutano-wa-apple

Kama jana ulikosa kuangalia uzinduzi wa simu mpya ya Apple iPhone 7 pamoja na iPhone 7 plus, yafuatayo ni matukio yote yaliyotokea hapo jana kwenye mkutano huo wa uzinduzi uliofanyika huko San Francisco’s Bill Graham Civic Auditorium.

Advertisement

Hapo jana tarehe 7 september 2016 kampuni ya Apple ilizindua simu zake mbili mpya ambazo zimetengenezwa kwa teknolojia mpya pamoja na maboresho mengi kama vile

Kamera

Kamera ya iphone 7 pamoja na 7 plus zimetengenezwa kwa kiwango cha 12MP lakini iphone 7 plus inayo kamera mbili zenye uwezo wa 12MP kila moja, pia uwezo wa ku-zoom wakati unachukua picha au video umeongenzwa mara 10 zaidi.

Spika

Spika za iphone 7 pamoja na 7 plus zimeongezewa uwezo ukilinganisha na toleo la iphone la mwaka jana (iphone 6) kwani sasa simu hiyo inauwezo wa stereo spika ikiwa na mana kuwa simu hiyo sasa inatumia spika mbili moja chini karibia na kipaza sauti (mic) na nyingine juu karibia na spika ya kusikilizia.

Vibonyezo

Vibonyezo vya iphone 7 pamoja na 7 plus vimetengenezwa kwa muonekano mpya kabisa, pamoja na kuongezewa teknolojia ya kisasa inayofanya vibonyezo hivyo kuwa bora zaidi kwani sasa kibonyezo maarufu cha (home button) kitakua hakibonyezeki kwa kubonyea bali kitakua kikitumia teknolojia ya kisasa kutambua kuwa umebonyeza yani (touch button)

Head phone

Kama wengi tulivyokua tunajua iphone 7 pamoja na 7 plus zimeamua kuachana na matumizi ya earphone zenye kutumia (earphone jack) na kuamia kwenye aina mpya ya (inlightin cable) ambayo itakua ikitu miaka kwenye earphone za sim hizo mpya, ila kama bado unataka kutumia earphone zako zenye kutumia earphone jack Apple wameweka waya maalumu wenye uwezo wa kuunganisha cable ya inlightin cable pamoja na earphone jack. Pia kama haitoshi Apple wamekuja na teknolojia mpya ya earphone ambazo zitakua zinaitwa EarPods earphone hizi ni wireless na zina mic kwenye kila spika hivyo zinawezo mkubwa wa kukusaidia kuongea au kusikiliza mziki kwenye simu yako bila kuishika simu yako, pia EarPods hizo zina kitufe maalumu cha kupokea simu pamoja na kufungua programu maalumu ya (Siri) kwenye simu yako.

Battery

Battery ya iphone 7 pamoja na 7 plus  zimeboreshwa zaidi kwani simu hizi sasa zinauwezo wa kudumu na chaji masaa mawili zaidi ya ile ya simu ya iphone 6 aliyotoka hapo mwaka jana.

Memory Capacity

Simu hizi sasa zimeongezwa ukubwa wa kiwango cha memory kwa kuongezewa memory kuanzia kiwango cha GB 32, GB 128 na GB 256 hivyo hakutakua na GB 16 maana yake ni kwamba iphone 7 yenye memory ndogo kuliko zote itaanzia GB 32.

Maboresho Mengine

Sasa simu hizi za iphone 7 pamoja na 7 plus zimekuja na uwezo mwingine wa kuzuia simu isichafuke na vumbi yani (dust resist) na pia kuzuia simu isingie maji yani (water resist).

SAA MPYA YA APPLE WATCH (SERIES 2)

Hapo jana pia Apple walizindua saa yao mpya ijulikanayo kama series 2 saa hii inasifa nyingi pamoja na teknolojia mpya ambayo imefanya saa hiyo kua moja kati ya saa za tofauti sana kutoka Apple. Pia kioo cha saa hiyo ni moja kati ya kioo angavu sana kuliko vioo vyote ambavyo kampuni hiyo inatumia kwenye bidhaa zake, hata hivyo saa hii inaendeshwa na processor mbili zenye nguvu ya kuendesha baadhi ya programu mpya ambazo zinapatikana ndani ya saa hiyo.

MFUMO MPYA WA UENDESHAJI WA iOS 10

Pia hapo jana Apple walitangaza kutoa toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa iOS 10 ambapo mfumo huo umeongezewa maboresho mengi kama vile Music Player ya sasa imeboreshwa, App Store imeboreshwa na kuongezewa App na Game mpya mbalimbali kutoka Apple, moja kati ya Game zilizo ongezwa ni pamoja na ujio wa game Mpya ya Super Mario kwenye iPhone pamoja na Pokemon Go kwenye Apple Watch, Hata hivyo toleo hilo jipya linategemewa kuwafikia watu kuanzia tarehe 13 september 2016, simu za iphone 7 pamoja na 7 plus zitakuja na mfumo huo mpya moja kwa moja.

Na hayo ndio matukio yote muhimu yalio jiri jana kwenye mkutano wa Apple Special Event uliofanyika hapo jana, kama unataka kuendelea kupata habari na matukio ya teknolojia endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use