Unapo nunua simu mpya hasa smartphone, yapo mambo mengi sana ya kuzingatia. Yafauatayo ni baadhi tu ya Mambo hayo muhimu ambayo ni vyema kufuatilia ili kufanya simu (smartphone) yako kudumu zaidi na kukaa na chaji kwa muda mrefu.
- Chaji Simu Yako
Watu wengi wanajua hili lakini watu wengi hawajui sababu za kufanya hivi, sababu za kuchaji simu yako kabla ya kuitumia ni kuangalia kuwa battery yako inadumu kwa muda gani. Mara nyingi mtu unapo nunua kitu kipya wengi wetu hujikuta tunatumia kitu hicho mara nyingi kwa sababu ni kipya hivyo usipo chaji simu yako ikajaa sababu unaitumia sana ni lazima utaona simu hiyo inaisha chaji mapema na huto jua simu hiyo ina uwezo gani kwenye upande wa battery. Kumbuka kuwa matumizi halisi ya simu yako ni pale tu unapo nunua simu hiyo, kwani baada ya hapo utakua unatumia tu sehemu unazo hitaji kutumia kwa muda huo kwa mfano, kuchat, kupiga simu na mengineyo.
- Hakikisha Ulinzi Kwenye Simu Yako
Baada ya kununua simu yako ni lazima uhakikishe ulinzi kabla ya hayo mengine kwani mara nyingi tunasahau kufanya hivi hivyo simu yako inapopotea unajikuta unajilaumu kwanini ukufanya hivyo mara ya kwanza. Kufanya hili hakikisha unawasha programu zote zenye kuweka ulinzi kwenye simu yako, kwa mfano unaweza kuwasha programu ya Android Device Manager kama unatumia simu ya Android au kama huitaji programu hiyo unaweza kuangalia programu zingine kupitia soko la Google Play hapa.
- Ondoa Programu Ambazo Huzitumii (Hutozitumia)
Programu nyingi zinazokuja na simu zinakuwa hazitumiki, kwa mfano ukiangalia simu yako kwa sasa je ni programu ngapi ambazo huzitumii.? kiukweli utakuta ni nyingi sana, sababu ya kuondoa programu hizo ni kuwa programu hizi zinatabia ya kutumia internet bila wewe kujua hivyo utakuta simu yako inaisha chaji au inapata moto kuliko kawaida japo ulikua hauitumii. Hivyo ni vyema kuondoa au kuzima kabisa programu hizo ili kusaidia chaji ya simu yako na kufanya matumizi bora ya data kwa kulinda bando lako, kwani ni mara nyingi sana unanunua bando na bila kujua unakuta limeisha ghafla.
- Panga Simu Yako Vizuri
Swala hili ni muhimu sana kwani ni muhimu kuweka simu yako kwenye mazingira ambayo utaweza kutumia simu yako kwa haraka, ukweli ni kwamba watu wengi simu zao haziko kwenye mpangilio kiasi kwamba ukiambiwa tafuta programu fulani kwenye simu yako inakuchukua muda mrefu. Hiyo yote ni sababu ya kukosa mpangilio kwenye simu yako.
- Update Programu na Simu yako kwa Ujumla
Hapa hakikisha simu yako na programu zake zote zipo kwenye hali nzuri ikiwa pamoja na kuwa zipo (up to date) au zipo kwenye matoleo ya sasa. Ni muhimu kwani kwa kufanya hivyo utakuwa umeweka simu yako kwenye hali ya kudumu.
Hayo ndio baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyafanya pale unapo nunua simu yako kwa mara ya kwanza, ni muhimu kuzingatia haya kwani itakupa uwezo wa kudumu na simu yako kwa muda mrefu.