Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Yahoo Yadukuliwa na Akaunti Bilioni Moja Zachukuliwa

Yahoo yatangaza kuwa imedukuliwa na kupoteza akaunti nyingi kuliko mtandao wowote ule duniani
Yahoo Yahoo

Kampuni ya teknolojia ya Yahoo ambayo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za barua pepe, hivi karibuni imetangaza kuwa imedukuliwa na kupoteza akaunti za wateja wake zaidi ya bilioni moja.

Katika sakata hili kampuni ya Yahoo imetoa taarifa hiyo ambayo inaonyesha mwaka 2013, kampuni hiyo ya teknolojia ili dukuliwa na kupoteza akaunti zaidi ya bilioni moja au hata zaidi. Yahoo inasema kuwa tukio hili linatofautiana kabisa na tukio lililotangazwa Mwezi September, ambapo ilitangazwa kuwa akaunti zaidi ya 500 ziliweza kudukuliwa.

Advertisement

Hata hivyo kampuni ya yahoo imesema kuwa kwa sasa imefika mahali pagumu, kwani kwa miaka yote hiyo imejitahidi kufanya kazi na polisi pamoja na wataalum mbalimbali ili kujua udukuaji huo ulipotokea, lakini mpaka sasa jitihada hizo zimeshindikana hivyo bado wahusika hawajakamatwa.

Vile vile Yahoo inasema kuwa imechukua hatua kadhaa za kuhakikisha akaunti za wateja wake zinakuwa zenye ulizi madhubuti, ikiwa ni pamoja na kuwataka wateja wake kubadilisha nywila (password) za akaunti zao. Kampuni hiyo inasema kuwa inahisi kuwa watu walio husika na shambulizi lililotangazwa mwezi september, ndio walio husika pia na shambulizi hilo la mwaka 2013.

Ni muhimu kukumbuka kubadilisha password yako kama bado hujabadilisha kwani huenda kuna watu wanasoma email zako na kutawanya nyaraka zako za siri kwenye mtandao, pia unaweza kuwa na (barua pepe) email zaidi ya moja ili kuepusha matatizo haya ya udukuzi kwenye mtandao. Unaweza kusoma taarifa kamili iliyotolewa na kampuni hiyo hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use