Hili limekuwa ni tatizo kubwa linalopitiwa takribani na kila mtu mwanafunzi shuleni, raia wa kawaida mtaani na pengine hata kwa aliyekazini ambaye kwa namna moja ama nyengine haridhishwi na sehemu anayofanyia kazi.
Hivyo basi kupitia XTOK event iliyofanyika jumamosi ya tarehe 21/8/2020 chini ya udhamini wa Infinix Mobile Limited na kuhudhuriwa na watu mbalimbali ikiwamo wanafunzi na wageni waalikwa.
Miongoni mwa wageni waalikwa ambao uthubutu wao ama kujitolea kufanya kazi bila ya malipo hapo awali ndio kumewafanya wawe na ajira za kudumu kwa sasa na miongoni mwao ni Bw. Frank na francis.
Hawa creative designer na walianza kufanya kazi hii wakiwa bado ni wanafunzi na katika kuongeza ujuzi walifanya bila ya kulipwa na sasa ni creative designer wakujiajiri.
Dr. Lilian Benjamini ni youth advocate kwa sasa, lakini alianzia chuoni kwa kujitolea katika shughuli za chuo na za mashirika mbalimbali, Bwa Elisha Simon CEO wa kampuni ya Neiked advertising, Bw Simon yeye uthubutu ndio umemfanya awe hapa alipo kwa sasa kwani hakuogopa kutake risk na hadi kufikia hatua ya kufungua kampuni akiwa shuleni, hivyo basi tunaona uthubutu na kujitolea ni miongoni mwa njia za kujipatia ajira.
Katika mdahalo huo wa tunapataje kazi kikwazo kilichoonekana kuwasumbua wengi ni namna ya kupata mtaji wa kuweza kujiajiri wengi wanafikiri ni pesa ila si kweli vipo vitu vingi vinaweza kukufanya ujiajiri alisema muendeshaji Event iyo hiyo ya XTOK kwa kujitolea mfano kupitia kazi yake ya utangazaji, haitaji mtaji mkubwa kuwa kama yeye bali ni kujiamini, kujifunza na kuthubutu.
Event ilikuwa ni ya kuelimisha na kufundisha wahudhuriaji walionekana kufuraiya mada ya tunapataje kazi na zawadi mbalimbali kutoka wadhamini Infinix Mobile Limited zilitolewa kwa wageni wote.