Intaneti ni moja wapo ya ugunduzi uliofanyika wa mafanikio makubwa sana, Intaneti imefanikiwa kufanya mapinduzi kwenye sekta ya teknohama na mawasliano.Tokea kuvumbuliwa kwa Simu,Kompyuta na Redio Intaneti imewezesha muingiliano wa mawasaliano kuwa mwepesi , imara na nafuu.Intaneti imesaidia kwa asilimia kubwa utandawazi kuenea.
Leo hii Intaneti imesambaa ulimwenguni kote ,historia yake ya uvumbuzi ilikuwa na vikwazo vingi kufikia wigo huu ulioenea duniani ilihusisha nyanja mbalimbali kama watalamu wa teknolojia kutoka sekta za mawasiliano pamoja na wataalamu wa kompyuta wakiwewmo hata wana sera wa jamii kufanikisha uwepo wake.
Tafrija ya X-TOK chini ya udhamini wa Infinix Mobility Tanzania uliofanyika jumamosi iliyopita ya tarehe 7 Disemba 2019 kwenye jukwaa la Sahara Ventures uliendeshwa kwa jadili mada isemayo “Je, ni nini muafaka wa biashara Intaneti ikizimika” ambapo ilifanyika kwenye mfumo wa majadiliano kati ya wageni wetu wasikilizaji na wageni wazungumzaji.
Tulibarikiwa na wageni wazungmzaji wenye uzoefu kwenye sekta zao za kazi na ujuzi miongoni mwao alikwemo Bw.Anthony Luvanda, Bi.Cynthia Bavo pamoja na Bw.Princely H.Glorious.
Wazungumzaji walikuwa na mengi ya kusema kuhusu mada husika, “Internet hutumika kama nyenzo ya mawasiliano katika biashara kwa ku sambaza taarifa kwa wateja wake, Bila Internet, Biashara nyingi sana zita anguka na kupelekea kudondoka kwa soko la ajira, alisikika Princely Glorius.
Mr. Luvanda akachangia kwa kusema, itakuwa ni changamoto kubwa kwa kampuni kurudi katika mbinu za mawasiliano za zamani au kuhamia kwenye mbinu itakayo kuwa mpya, hii itaumiza Biashara nyingi.
Kuwa mzazi na mfanyakazi ni ngumu kwa hali ya kawaida, lakini kutokana na uwepo wa nyenzo za Internet hurahisisha changamoto hizi, Pia internet hutumika kama chanzo cha Buudani, Tunatumia Internet kujifunza mambo mengi mtandaoni hivyo kukosekana kwa Internet kutaleta udororaji katika sekta mbalimbali alisikika Cynthia Bavo (Mmoja wa wageni waalikwa)
Jukwaa lilikuwa kimya kutafakari hoja hizi kutoka kwa washiriki na pia kuchangia mawazo mbalimbali. Naamini Historia imefanya kazi ya kutambua tulipotoka, tulipo na kutabiri tunapoelekea, na kwa tulipo toka mpaka sasa Internet imeleta mapinduzi makubwa katika Biashara, hivyo kuzimika kwa Internet kutaleta maafa katika Biashara, mmoja ya wageni wasikilizaji alichangia kwa hisia.
XTOK Ili wazawadia wazungumzaji wasikilizaji waliokuwa wakichangia mada zaidi, mmoja aliondoka na Infinix S5 Mpya pamoja na zawadi nyingine nyingi.
XTOK Hufanyika mara 3 kwa mwaka, event ifuatayo inatarajia kufanyika mwezi wa tatu mwaka 2020. Lengo kuu la Event hii ni kukutanisha vijana wenye kiu ya maendeleo na ubunifu kuanzia ngazi ya elimu ya juu mpaka wafanyakazi na wajasiriamali mbali mbali, ili kuleta mtazamo chanya juu ya Teknolojia, ubunifu na maendeleo