Wakati bado asilimia kubwa ya watanzania wakiwa wanatumia mfumo wa Windows 7 kwenye kompyuta zao, hapo kesho mfumo huo unaenda kusitishwa rasmi na kampuni ya Microsoft kama ilivyo tangazwa hapo mwaka jana 2019.
Kwa mujibu wa Microsoft, mfumo wa Windows 7 utasitishwa kupewa update mbalimbali za kawaida pamoja na update za ulinzi ambazo zimekuwa zikipakiwa kwenye mfumo huo mara kwa mara. Hata hivyo mbali ya kusimamishwa kwa update hizo, kwa mujibu wa tovuti ya how to geek, mfumo huo wa Windows 7 unaweza kukosa uwezo wa kuendesha baadhi ya programu za muhimu mara baada ya kusitishwa rasmi, japo kuwa inaweza kuchukua muda mrefu.
Hata hivyo Microsoft imeithinisha kuwa, mfumo wa Windows 7 unaweza kuendelea kutumika kama kawaida, lakini mtumiaji hatoweza kupata update hizo ambazo ni muhimu kwa usalama wa mtumiaji kwani huzuia mfumo huo kutokudukuliwa (hacked). Hivyo kwa kuendelea kutumia mfumo huo, uwezekano wa kudukuliwa au kuwa-hacked ni mkubwa sana kutokana na mfumo huo kukosa update hizo za muhimu.
Kwa sasa kama wewe ni mtumiaji wa Windows 7, unatakiwa kuhakikisha una update kwenda kwenye mfumo wa Windows 10 kama kompyuta yako inayo uwezo wa kuendesha mfumo huo. Kama kompyuta yako inayo uwezo huo basi unaweza kubofya hapa kisha soma maelezo ili kusasisha mfumo huo bure bila kulipia.
Kama ulikua unajiuliza…!, hapo siku ya kesho hakuna mabadiliko yoyote utakayo yaona kwenye mfumo huo, bali kuanzia siku ya kesho hutoweza kupata update zozote kwenye mfumo huo.
Maoni*kwaiyo windows ya kutimia ni windows ip?
Windows 10