WhatsApp imetangaza kipengele kipya kitakachowaruhusu watumiaji kuhifadhi mawasiliano ndani ya programu ya WhatsApp. Hii inamaanisha kwamba hata kama ukipoteza simu yako au ukiunganisha kifaa kipya kwenye nambari yako kuu, utaona mawasiliano yako yote yaliyohifadhiwa kwenye hifadhi ya WhatsApp.
Hadi sasa, WhatsApp ilikuwa inategemea mawasiliano ya ndani ya simu yako (Phonebook) tofauti na itakavyokuwa hivi karibuni.
Kipengele hicho kipya, kinakuruhusu kuhifadhi mawasiliano kwenye hifadhi ya WhatsApp, na utaweza kutumia majina hayo popote ikiwa ni pamoja na WhatsApp kwa wavuti na Windows. Unaweza pia kuchagua kuweka majina yatakayokuwa kwenye WhatsApp Cloud kuja kwenye simu yako.
WhatsApp ilisema ilibuni mfumo mpya wa uhifadhi unaoitwa Identity Proof Linked Storage (IPLS) ili kuwezesha kuhifadhi mawasiliano kwa usalama. Wakati watumiaji wanapohifadhi mawasiliano, mfumo huo utatengeneza uthibitisho maalum kulingana na kifaa ili kuzuia mtumiaji yoyote kufanya mabadiliko yasiyo rasmi kwenye mawasiliano
Aidha, programu inashirikiana na Cloudflare kuweza kufanya sehemu hii kuwa na ulinzi zaidi na usalama kwa watumiaji wote.
Hata hivyo Kampuni hiyo ilisema kuwa teknolojia iliyopo nyuma ya kipengele cha kuhifadhi mawasiliano itamwezesha mtumiaji kuhifadhi mawasiliano pia kwa kutumia username.
“Username kwenye WhatsApp itaongeza kiwango cha faragha na itasaidia pale ambapo huitaji kushiriki namba yako ya simu wakati wa kutuma ujumbe kwa mtu,” kampuni hiyo ilibainisha katika chapisho la blog. Kipengele hicho kimekuwa katika majaribio. Mwezi Mei 2023, kwa mujibu wa ripoti ya WABetaInfo.