Kampuni ya facebook kupitia blog yake ya WhatsApp Blog imetangaza kukamilika kwa ulizi maalum wa watumiaji wa application hiyo ya WhatsApp. Blog hiyo imeandika ikifafanua ya kuwa sasa watumiaji wa application hiyo watakua na uwezo wa kutumiana meseji ambazo zitakua na ulizi wa hali ya juu sana hii ikiwa na maana kuwa meseji hizo za whatsapp hazita hifadhiwa kwa njia ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali bali sasa zitahifadhiwa zikiwa kwenye mfumo maalumu ambapo mtumiaji mwenyewe ndio atakae weza kuruhusu mtu au watu kusoma meseji hizo kutoka katika server ya Whatsapp.
Maboresho haya yamekuja wakati kampuni ya simu ya Apple pamoja na Askari maalumu wa ulinzi wa marekani yani FBI wakiwa wako kwenye sakata zito linalo husu ulinzi wa nyaraka za mtumiaji wa simu hiyo ya Apple, ambapo askari hao walikua wakitaka kuangalia nyaraka za simu za mtu anaetuhumiwa kuwa ni gaidi.
Hata hivyo WhatsApp inaendelea kuandika kwenye blog yake kuwa kama unatumia toleo jipya la sasa la application hiyo ya Whatsapp huna haja ya kufanya chochote ila ukumbuke pia meseji unayotuma inasomwa na mtu pekee anaye pokea meseji hiyo na wala si watu wengine.
Kwa maelezo zaidi pitia Blog ya WhatsApp hapa > https://blog.whatsapp.com