Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Programu ya WhatsApp Yafikisha Watumiaji Bilioni 1 kwa Siku

Sasa watumiaji wa programu ya Whatsapp Waongezeka kwa kasi
Whatsapp watumiaji bilion 1 Whatsapp watumiaji bilion 1

Programu ya WhatsApp hivi karibuni imefanikiwa kufika hatua kubwa sana kwa kuwa na watumiaji zaidi ya bilioni 1 duniani kote. Watumiaji hao ni wale wanao tumia programu hiyo kila siku hivyo ni sawa na kusema watumiaji wanaotumia programu hiyo kwa siku moja ni zaidi ya watu bilioni 1.

Kukuwa kwa watumiaji wa programu hii ni ishara tosha kuwa kampuni ya facebook inaongoza kwa upande wa programu za kijamii za kidigitali, mwezi huu facebook yenyewe ilifikisha watumiaji zaidi ya billioni 2 kwa mwezi wakati mtandao wa instagram ukiwa na watumiaji zaidi ya Millioni 700 kwa mwezi.

Advertisement

Hata hivyo programu hiyo ya whatsapp inafanya kazi ya kutumia picha zaidi ya bilioni 4.5 kwa siku na vilevile programu hiyo hutuma video zaidi ya Bilioni 1 kila siku. Mtandao huo bado unaendelea kukuwa na matumizi ya mitandao hiyo ya kijamii yana endelea kuongezeka kila siku tena hasa kwa nchi za afrika ambako matumizi hayo yanaonekana kukuwa kwa kasi.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : WhatsApp Blog

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use