Mwaka 2014 kampuni ya Facebook ilitangaza kununua WhatsApp kwa dollar za marekani Bilioni $21.8 ambayo ni takribani Shilingi za kitanzania TZS Trilioni 50.3 (50,358,000,000,000). Kwa kipindi hicho huu ndio ununuaji mkubwa uliohusisha kiwango kikubwa cha pesa.
Kipindi hicho cha nunuaji WhatsApp ilikuwa na jumla ya watumiaji zaidi ya milioni 500 ambapo sasa namba hiyo inaonekana kuongezeka kwa kasi. Mwaka 2016 app hiyo ilikuwa na jumla ya watumiaji Bilioni 1 na baadae mwaka 2018 WhatsApp ilifikisha jumla ya watumiaji bilioni 1.5.
Kupitia blog yake, WhatsApp imeandika kuwa hivi karibuni imefanikiwa kufikisha jumla ya watumiaji bilioni 2 kote duniani. Watumiaji hawa ni jumla ya watumiaji wote wa programu hiyo ikiwa pamoja na watumiaji wa app za mifumo yote ya Android pamoja na iOS.
Hata hivyo bado haija julikana kama jumla ya watumiaji hao bilioni 2 inajumuisha watumiaji wa programu ya WhatsApp Business.