Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sasa Utaweza Kushare WhatsApp Status Kwenye Facebook Stories

Hivi karibuni utaweza kushiriki status zako WhatsApp kwenda Facebook
Sasa Utaweza Kushare WhatsApp Status Kwenye Facebook Stories Sasa Utaweza Kushare WhatsApp Status Kwenye Facebook Stories

Wakati sehemu ya WhatsApp Status ikiwa iko mbioni kuanza kutumika kuonyesha matangazo, hivi karibuni Facebook kupitia app yake ya WhatsApp imeanza kufanya majaribio ya sehemu mpya itakayo ruhusu kushare WhatsApp Status kwenye Facebook Stories.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, sehemu hiyo mpya itamruhusu mtumiaji wa programu ya WhatsApp kuweza kushiriki (share) Status za WhatsApp moja kwa moja kutoka kwenye WhatsApp kwenda kwenye sehemu ya Facebook Stories kwenye akaunti ya mtumiaji husika.

Advertisement

Sasa Utaweza Kushare WhatsApp Status Kwenye Facebook Stories

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, kupitia sehemu hiyo pia utaweza kushare Status za WhatsApp moja kwa moja kwenye mitandao mingine kama vile Instagram, YouTube, Gmail pamoja na Google Photos. Hata hivyo Facebook imedai kuwa huna haja ya kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp na mtandao wa Facebook ili kuweza kushare Status kwenye mtandao huo.

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, sehemu hiyo mpya ya kushare status itakuwa inaonekana ndani kwenye programu ya WhatsApp kwenye uwanja wa Status chini ya picha ya status yako.

Kwa sasa inasemekana sehemu ya WhatsApp Status inatumika na zaidi ya watu milioni 500 kila siku, ndio maana Facebook imechagua sehemu hiyo kuwa ya kwanza kuonyesha matangazo hapo ifikapo mwakani 2020. Pengine juhudi hizi za kuunganisha Facebook na WhatsApp ni hatua ya awali ya kuandaa sehemu hiyo kwa ajili ya kuonyesha matangazo kwenye app ya WhatsApp.

Kwa sasa sehemu hiyo ya kushare Status bado haipatikani kwenye programu ya kawaida ya WhatsApp hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza pindi sehemu hiyo itakapokuja kwa watumiaji wote wa programu ya WhatsApp.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use