Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Programu ya WhatsApp Sio Salama Kama Unavyodhani

Hakuna ulinzi wa asilimia 100 kwenye programu ya whatsapp
Ulinzi wa WhatsApp Ulinzi wa WhatsApp

Siku ya ijumaa ya tarehe 13 tovuti maarufu ya habari ya The guardian ya nchini marekani iliandika makala maalum iliyokua ikitoa taarifa kuwa, sasa programu ya Whatsapp sio salama kwani kuna uwezekano wa wadukuzi au hata serekali kuingia kwenye programu hiyo na kufanya chochote wanachotaka ikiwemo kusoma meseji zako pamoja na mambo mengi.

Hata hivyo haikuchukua muda mrefu kampuni ya whatsapp ilitoa maelezo kwa kukanusha kuwa, hakuna tatizo la ulinzi kwenye sehemu yoyote kwenye programu hiyo (backdoor) wala sio kweli kwamba wadukuzi au serikali ina weza kusoma meseji za wateja wa programu hiyo yaani Whatsapp, wasemaji wa kampuni hiyo waliendelea kwa kusema kuwa inathamini ulinzi wa wateja wake na itapambana na haitatoa taarifa zozote zile za wateja wake kwa serikali au mtu yoyote itayetaka kufanya hivyo kwa namna yoyote ile, iwe kwa iyari au kwa kulazimishwa.

Advertisement

Kwa upande wa pili makala ya tovuti hiyo ya The guardian iliendelea kuandika kuwa, kwa muda sasa sehemu hiyo yenye ulinzi dhaifu imekua ikijulikana na kampuni ya Whatsapp, lakini kampuni hiyo haijawahi kufanya lolote ili kuboresha ulinzi wa programu hiyo. Katika sehemu nyingine ya makala hiyo ya The Guardian iliandika kuwa, ulinzi wa sasa uliopo kwenye programu ya Whatsapp hauto weza kuzuai shambulizi zilijulikanalo kama “Plausible Attack”, shambulizi hili ni pale wadukuzi wanapopata uwezo wa kuingia kwenye programu hiyo na kubadilisha namba maalum za ulinzi (encryption key) na kuwa programu maalum ya kusoma meseji zinazotumwa kati ya watumia wa programu hiyo.

Kwa sasa bado kuna mvutano na majadiliano makubwa kuhusu ulinzi wa programu hiyo maarufu duniani. Lakini mwisho ni kwamba mi nadhani kadri teknolojia inavyokuwa ndivyo ulinzi unavyokuwa ni mgumu kuwa wa uhakika hasa kwenye vifaa na programu za siku hizi. Tuna haja ya kurudi nyuma kidogo na kuanza kuchukua hatua za mara moja za kujilinda wenyewe bila kutegemea ulinzi kutoka kwenye makampuni yaliyotengeneza bidhaa au programu hizo.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu sakata hili la ulinzi wa programu ya WhatsApp unaweza kutembelea tovuti ya The Guardian, Pia kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store ili kupata habari zote za Teknolojia kwa haraka zaidi.

3 comments
  1. It’s pretty worth enough for me. In my view, if all web owners
    and bloggers made good content as you did, the net will
    be a lot more useful than ever before.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use