Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

WhatsApp Imeleta Mabadiliko Mapya ya Magroup ya WhatsApp

Sasa utaweza kutuma meseji “Private” ndani ya Magroup
reply privately reply privately

Moja kati ya sehemu ambayo hutumika zaidi kwenye programu ya WhatsApp ni pamoja na sehemu ya Magroup. Sehemu hii inakupa urahisi wa kuchati kwa pamoja na ndugu jamaa na marafiki pia inakupa muda wa kuweza kujifunza mambo mbalimbali.

Sasa kwa kuwa sehemu hii inahusisha marafiki, ndugu au jamaa, ni wazi kuwa kuna wakati unataka kuchata na mtu mmoja ndani ya group na hii ni mpaka utoke ndani ya group utafute namba ya mtu huyo uhifadhi kwenye simu yako ndipo uweze kuwasiliana na mtu huyo private.

Advertisement

Ni kweli kuwa hatua hizi huleta usumbufu mkubwa kwani kuna wakati unakuta unataka kuwasiliana na mtu ndani ya group mara moja tu na wala uhitaji ku-save namba yake. Sasa WhatsApp imeliona hilo na hivi karibuni inakuja na sehemu mpya ambayo itakuwezesha kuchat na mtu mmoja ndani ya group bila ku-save namba yake.

Kupitia sehemu hiyo mpya inayoitwa “Reply privately”, utakuwa na uwezo wa kumjibu mtu meseji ya ndani ya group bila watu wengine waliopo ndani ya group hilo kuweza kuona meseji hiyo.

Sehemu hiyo ambayo kwa sasa iko kwenye hatua za majaribio, itakuwa inapatikana pale unapokuwa unachat ndani ya group na kama unataka kujibu meseji ya mtu ndani ya group na hutaki watu wengine waone meseji hiyo. Utashikilia meseji unayotaka kujibu ndani ya group kisha utachagua sehemu ya “Reply Privately” inayo tokea juu upande wa kulia, kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu.

Kama nilivyo sema hapo awali, sehemu hii ya “Reply Privately” kwa sasa inapatikana kwenye toleo la majaribio la WhatsApp Beta, hivyo ni wazi kuwa itachukua muda kidogo hadi kuweza kuona sehemu hii kwenye programu ya kawaida ya WhatsApp.

Kwa sasa unaweza kutegemea kuona sehemu ya mpya ya stika, ambayo imetangazwa kuja siku za karibuni, sehemu ambayo itakuruhusu kutuma na kupokea stika kwa urahisi ndani ya programu ya WhatsApp. Kama unataka kujua zaidi kuhusu sehemu hii unaweza kusoma makala iliyopita hapa.

Kwa habari zaidi kuhusu mabadiliko mengine ndani ya programu ya WhatsApp usiache kutembelea Tanzania Tech kila siku pia hakikisha una download app yetu inayopatikana kwenye soko la Play Store pamoja na App Store.

1 comments
  1. Hiyo sehemu ya “reply privately” tayari inapatikana kwenye whatsapp ya kawaida.
    Mi natumia galaxy s6 (sprint).

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use