Kampuni ya maarufu ya facebook kupitia programu yake ya WhatsApp hivi karibuni imekua ikiandaa toleo lake jipya la whatsapp ambapo sasa watumiaji watakua na uwezo wa kufunga meseji kwa kutumia maneno maalumu ya siri (password)
Habari kutoka katika mtandao wa Android Authority zinasema kuwa huwenda sehemu hiyo mpya ikaja kwenye toleo jipya la whatsapp siku za usoni japo kampuni hiyo haijadhibitisha kuwa ni lini. Hata hivyo tovuti hiyo iliendelea kuandika kuwa sehemu hiyo mpya itakuja na sehemu nyingine maalum ya kurudisha password kwa njia ya barua pepe, hii ni pale utakapo kuwa umepoteza au umesahau password yako.
Hii itakuwa ni mara ya pili sasa kwa programu hiyo kuongezewa ulinzi zaidi baada ya mara ya kwanza programu hiyo kuongezewa ulinzi maalum wa (end-to-end encryption) mapema mwaka huu.
Kama unataka kupata habari ni lini sehemu hii itakuja kwenye programu yako ya Whatsapp.! endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.