Kwa muda mrefu imekuwa ni rahisi sana mtu kusoma meseji zako za WhatsApp hasa pale anapo fanikiwa kushika simu yako. WhatsApp imekuwa ikipokea malalamiko ya aina hii kwa muda mrefu na sasa inajiandaa kuja na suluhisho.
Hivi karibuni watumiaji wa WhatsApp wataweza kuona sehemu mpya ya Touch ID, sehemu hii itakuwa inaruhusu watumiaji wa simu mbalimbali zenye ulinzi wa kutambua uso au Face ID pamoja na ulinzi wa kutumia alama za vidole fingerprint kufungua meseji zao kwa kutumia ulinzi huo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Wabetainfo, sehemu hiyo itakuwa inapatikana kwenye sehemu ya privacy settings na pale inapowashwa basi mtumiaji ni lazima kuingiza password au kutumia Face ID au Fingerprint ndipo aweze kusoma kila meseji anayopokea kutoka kwa mtu.
Hapo awali njia ya kuzuia mtu asiweze kusoma meseji zako ilikuwa ni kwa kutumia programu maalum ambazo hizi huweka ulinzi wa pattern au ulinzi wa kutambua uso, lakini tofauti na programu hizi sehemu ya Touch ID itakuwa inataka uweze kuweka password kila mara unapo pokea meseji mpya na pale simu yako inapokuwa ilizima kioo chake au ulitoka kwenye programu hiyo.
Bado hakuna taarufa zaidi ya lini sehemu hii itakuja rasmi kwenye programu ya WhatsApp, lakini pengine siku sio nyingi kwani kwa sasa sehemu hiyo iko kwenye hatua za majaribio. Kujua zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
Maujanja : Jifunze Jinsi ya Kuzuia Mtu Kusoma Meseji Zako za WhatsApp Unapokuwa Kwenye Mkusanyiko wa Watu.