Programu ya WhatsApp hivi karibuni imekua ikiongezewa sehemu mpya ambazo hufanya programu hiyo kuwa rahisi kutumia na pengine muhimu kuwa nayo. Katika kuboresha zaidi programu hiyo, WhatsApp imepanga kuja na sehemu mpya yenye kukupa uwezo wa kuona mahali mtu alipo kwa kutumia ramani, sehemu hiyo iliyopewa jina la Live location inategemewa kuja hivi karibuni kwa watumiaji wote wa programu hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya teknolojia ya Tech2.com sehemu hiyo itakuwa pekee kwenye magroup ambapo hapo ndipo utaweza kuwasha sehemu hiyo kwa kubofya option ya ‘Show my friends’ iliyoko kwenye group kisha baada ya hapo utapewa uwezo wa kuchagua muda ambao unataka watu waweze kuona ulipo. Utaweza kuchagua kati ya dakika moja, dakika mbili, dakika tano au kuiwasha sehemu hiyo moja kwa moja.
Sehemu hiyo mpya itakuwa inaendeshwa na ramani ya Google Map ambapo mtu akitaka kuona mahali ulipo atabofya mahali palipo andikwa ‘Show my friends’ na kwa kufanya hiyo ramani ya Google itafunguka na kukuonyesha marafiki zako waliowasha sehemu hiyo walipo. Hata hivyo kwa sasa sehemu hiyo mpya ya Live Location inategemewa kutoka pekee kwaajili ya magroup na bado haijajulikana kama sehemu hiyo itapatikana pia kwa mtu mmoja mmoja ndani ya programu hiyo.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una pakua App ya Tanzania Tech kupitia Play Store ili kupata habari zote mpya za teknolojia kwa haraka. Pia kama unataka kujifunza mambo mbalimbali pamoja na kupata habari kwa video unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube.
Hiyo ije kwani itasaidia katika wimbi la udanganyifu na mengineyo mengi.
Nimependa sana blog yenu
Asante Sana Mtu
poa msaada mzur sana
Karibu sana
nisaidien jaman nataka ni danlond whtasapp kwenye computer nasshindwa nisaidien jaman nifanyaje