Kama umekuwa mtumiaji wa WhatsApp kwa muda mrefu ni wazi umeshapitia kitendo cha kupata meseji nyingi kwa muda mfupi kutoka kwa mtu mmoja. Mara nyingi meseji hizi zinakuwa sumbufu kwa sababu wakati huo unakuta labda huwezi kusoma meseji hizo kutokana na kuwepo mahali fulani panapo hitaji faragha.
WhatsApp imeliona hili na sasa inakuja na njia mpya kabisa ya kuweza kuzuia kupokea meseji nyingi kutoka kwa mtu mmoja, a.k.a meseji sumbufu ambazo kwa wakati huo unakuta huwezi kuzisoma. Sehemu hii mpya itakuwezesha kuzima au (Ku-Mute) ujumbe taarifa au (Notification) moja kwa moja kwenye pazia la ujumbe kabla ya kufungua meseji yenyewe.
Sehemu hii mpya itatokea upande wa kulia pembeni na sehemu ya REPLY ambayo huonekana kwa juu kwenye pazia la taarifa za WhatsApp kwenye simu ya Android. Hata hivyo ili kusudi sehemu hiyo iweze kutokea, inabidi uwe umepokea meseji hizo sumbufu zaidi ya 50 ndipo uweze Ku-Mute ujumbe taarifa huo kwa kubofya sehemu hiyo mpya ya MUTE ambayo itapatikana kwenye pazia la taarifa za WhatsApp.
Kwa sasa sehemu hii bado iko kwenye toleo la majaribio la WhatsApp Beta na inategemewa sehemu hii itakuja kwa watumiaji wote wa simu za Android siku za karibuni.
Mbali na hayo hivi karibuni pia watumiaji wa programu ya WhatsApp wataweza kufurahia sehemu mpya ya Stickers, ambayo itaruhusu watumiaji kuweza kutumiana meseji mbalimbali kwa kutumia Sticker mbalimbali ndani ya programu ya WhatsApp. Vilevile inasemekana kuwa sehemu hiyo itakuja na sehemu mpya ya Sticker Store ambayo utaweza kuitumia kupakua (Download) na kusasisha (Update) sticker mpya pale utakapo hitaji.
WhatsApp beta for Android 2.18.218:
[STICKERS WILL BE AVAILABLE IN FUTURE – NO RELEASE DATE AVAILABLE!!!] pic.twitter.com/m86vLp28zB
1) Sticker preview!
2) When the WhatsApp Sticker Store has a new updated sticker pack, there will be a green dot on the “+” button.
3) Added the update button.— WABetaInfo (@WABetaInfo) July 16, 2018