Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

WhatsApp Kuacha Kufanya Kazi Kwenye Simu Hizi (November)

Kama unatumia simu moja kati ya hizi basi ni wakati wa kubadilisha simu
WhatsApp Kuacha Kufanya Kazi Kwenye Simu Hizi (November) WhatsApp Kuacha Kufanya Kazi Kwenye Simu Hizi (November)

Mwaka 2021 umekaribia kuisha, hii inaonyesha mwanzo wa programu ya WhatsApp kuacha kufanya kazi kwenye baadhi ya simu za zamani.

Hili sio jambo jipya sana, kwani huu umekuwa ni utaratibu wa WhatsApp kila mwaka kutangaza kuacha kufanya kazi kwenye baadhi ya simu za zamani.

Advertisement

Mwaka huu listi ya simu hizo imeongezwa kidogo pia vilevile ikiwa na baadhi ya simu za iPhone zenye mfumo wa zamani wa iOS.

Kwa mujibu wa WhatsApp, ifuatayo ndio list ya simu kwa mwaka huu 2021, simu ambazo zinasemekana kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi kwenye programu ya WhatsApp kuanzia tarehe 1 November 2021.

WhatsApp Kuacha Kufanya Kazi Kwenye Simu Hizi (November)

List ya Simu Ambazo Hazitakuwa na Uwezo wa Kutumia App ya WhatsApp mwaka huu 2021 kuanzia tarehe 1 mwezi Novemba ni kama ifuatavyo.

Simu za Apple

Kuanzia November, WhatsApp haita fanya kazi kwenye simu zote za iPhone ambazo zinatumia mfumo wa iOS 9. Hivyo kama simu yako haitakuwa na uwezo wa kupokea mfumo wa iOS 10, basi moja kwa moja haito kuwa na uwezo wa kutumia WhatsApp. Kwa sasa simu hii ni iPhone 4S ambayo ilizinduliwa mwaka 2011.

Simu nyingine kama iPhone SE (2016), iPhone 6S, na 6S Plus ambazo zilizotoka na mfumo wa iOS 9 zina weza kupokea mfumo mpya wa iOS 15.

Simu za Samsung

Simu za Samsung ambazo hazitoweza kutumia mfumo programu ya  WhatsApp kuanzia November ni pamoja na :

  • Samsung Galaxy Trend Lite
  • Galaxy Trend II
  • Galaxy SII
  • Galaxy S3 mini
  • Galaxy Xcover 2
  • Galaxy Core
  • Galaxy Ace 2.

Simu za Sony

Simu za Sony ambazo hazitoweza kutumia programu ya WhatsApp baadae mwaka huu ni pamoja na:

  • Sony Xperia Miro
  • Sony Xperia Neo L
  • Xperia Arc S.

Simu za Huawei

Soma hapa kujua list ya simu za Huawei ambazo hazitoweza kutumia programu ya WhatsApp.

  • Huawei Ascend G740
  • Ascend Mate
  • Ascend D Quad XL
  • Ascend D1 Quad XL
  • Ascend P1 S
  • Ascend D2.

Simu za ZTE

Simu za ZTE ambazo haziwezi kupokea mfumo wa  Android 4.1 hivyo hazitakuwa na uwezo wa kutumia programu ya WhatsApp :

  • ZTE Grand S Flex
  • ZTE V956
  • Grand X Quad V987
  • Grand Memo.

Simu za LG

  • LG Lucid 2
  • Optimus F7
  • Optimus F5
  • Optimus L3 II Dual
  • Optimus F5
  • Optimus L5
  • Optimus L5 II
  • Optimus L5 Dual
  • Optimus L3 II
  • Optimus L7
  • Optimus L7 II Dual
  • Optimus L7 II
  • Optimus F6
  • Enact
  • Optimus L4 II Dual
  • Optimus F3
  • Optimus L4 II
  • Optimus L2 II
  • Optimus Nitro HD
  • 4X HD
  • Optimus F3Q.

Simu Nyingine

  • Alcatel One Touch Evo 7
  • Archos 53 Platinum
  • HTC Desire 500
  • Lenovo A820

Vilevile inasemekana simu za Android ambazo zitakuwa zinatumia mfumo wa Android 4 kushuka chini zitashindwa ku-support programu ya WhatsApp kuanzia mwaka 2022.

Pia ripoti hiyo inasema kuwa simu zote iPhone zinazotumia mfumo wa iOS 9 pia hazi takuwa na uwezo wa ku-support programu hiyo ifikapo mwezi February mwaka 2022.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use