Tetesi : WhatsApp Kuja na Programu Mpya Kwaajili ya Kompyuta

Programu mpya ya kompyuta itakuwa inaweza kutumika bila simu
Tetesi : WhatsApp Kuja na Programu Mpya Kwaajili ya Kompyuta Tetesi : WhatsApp Kuja na Programu Mpya Kwaajili ya Kompyuta

WhatsApp ni moja kati ya programu bora za kuchati zinazotumiwa na watu wengi zaidi duniani, hadi mwezi wa nne mwaka huu 2019 programu hiyo imefikisha watumiaji zaidi ya bilioni 1.6 kwa mwezi, huku india ikiwa inashikilia namba moja kwa kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 400.

Katika kuendeleza kujuhudi za kufanya programu hiyo kutumiwa zaidi, hivi karibuni tetesi zimeibuka zikidai kuwa WhatsApp inafanya maandalizi ya kuja na programu mpya ya WhasApp kwaajili ya Kompyuta. Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya WABetaInfo, Programu hiyo mpya ni tofauti kabisa na programu ya sasa ambayo nilazima simu yako iwe hewani ndipo uweze kuitumia.

Advertisement

Kwa mujibu wa ripoti hiyo inasemekana programu hiyo mpya kwaajili ya kompyuta itakuwa na uwezo wa kutumiwa bila kuunganisha simu, hivyo kuruhusu watu kuweza kuchat kwa kutumia kompyuta bila kuunganisha na simu kama ilivyo kwenye programu ya sasa.

Kwa sasa bado hakuna ripoti zaidi juu ya programu hiyo mpya lini itakuja hivyo hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi kuhusu hilo. Kama unataka kujua zaidi kuhusu WhatsApp, unaweza kusoma hapa kujua maujanja ya jinsi ya kutumia WhatsApp kwa njia za kisasa zaidi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use