Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye hivi leo WhatsApp imewezesha ulinzi wa alama za vidole kwenye App yake ya mfumo wa iOS. Kwa mujibu wa tovuti ya 9to5mac.com, sehemu hiyo sasa inapatikana kwenye toleo jipya la programu ya WhatsApp ya iOS yenye toleo namba 2.19.20.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, sehemu hiyo haitofanya kazi kwenye chat moja moja, bali itakuwa inaongeza ulinzi kwenye programu nzima ya WhatsApp pale unapotaka kufungua app hiyo kwenye simu yako. Hata hivyo watumiaji wataendelea kuona meseji ambazo hutokea kwenye sehemu sehemu ya notification lakini hautoweza kusoma meseji nzima hadi kuweka password au alama za vidole au Face ID kwa simu zenye uwezo huo.
Kwa sasa sehemu hii bado haijatangazwa kwenye programu ya Android, ila pengine kwenye siku chache zinazokuja tegemea kuona sehemu hii. Kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp ya iOS, ili kupata sehemu hii hakikisha una update kwana toleo jipya la WhatsApp kupitia App Store, kisha baada ya hapo ingia ndani ya programu ya WhatsApp kwenye sehemu ya Settings –> Account –> Privacy kisha washa sehemu ya Screen Lock.
Kwa watumiaji wa Android endelea kutembelea Tanzania Tech tutawajulisha pindi sehemu hii itakapo fika rasmi kwenye programu hiyo. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una tembelea Tanzania Tech kila siku.