Ikiwa imepita muda mrefu toka tusikie kuhusu kuongezwa kwa sehemu mpya kwenye App ya WhatsApp ya mfumo wa iOS, hivi karibuni watumiaji wa mfumo huo wataenda kuona mabadiliko kadhaa ambayo yanakuja na toleo jipya la programu ya WhatsApp ya mfumo wa iOS.
Mabadiliko hayo mpya yanategemewa kuonekana kwenye toleo la WhatsApp la mfumo wa iOS lenye version namba 2.18.90, Pia inasemekana kuwa madiliko kwenye toleo hilo yatakuwa ni kwaajili ya mfumo wa iOS ambao una anzia iOS 8 kuendelea, hivyo kwa wale watumiaji wa iOS 7 hawatoweza kuona mabadiliko haya mpya.
- Sasa Utaweza Kutafuta Status
Kupitia toleo hilo jipya WhatsApp imeleta sehemu mpya ambayo itawawezesha watumiaji wa programu hiyo wa mfumo wa iOS kuweza kufauta Status ya mtu moja kwa moja kupitia sehemu ya Status. Sehemu hiyo itawezeshwa na sehemu ya kutafuta ambayo imeongezewa kwenye sehemu ya Status ndani ya programu ya WhatsApp.
- Sasa Utaweza Kuangalia Picha Kabla ya Kufungua App ya WhatsApp
Sehemu hii tulishawahi kuizungumzia kwenye makala iliyopita na kama ukusoma makala hiyo, sehemu hii inaleta uwezo wa kuangalia picha pamoja na GIF moja kwa moja kupitia sehemu ya Notification hata kabla ya kufungua ujumbe wenyewe kupitia App ya WhatsApp.
- Sasa Utaweza Kujua Link Zisizo Salama Kabla ya Kuzifungua
Sehemu nyingine ambayo inakuja kwenye toleo hili jipya ni pamoja na sehemu ya kujua link zisizo salama kabla ya kuzifungua au Suspicious Link. Sehemu hii kama ilivyo sehemu iliyopita tulishawahi kuizungumzia kwa watumiaji wa Android na sasa sehemu hii inakuja kwenye mfumo wa iOS. Kama ukusoma makala hiyo, sehemu hii itakupa uwezo wa kuonyesha alama ya hatari juu ya link ambayo umetuma au umetumiwa ili kuonyesha kuwa ni tovuti yenye link hiyo ni hatari au hiyo website yenyewe kutokuwa salama.
Na hayo ndio mabadiliko mapya yanayo tarajiwa kuja hivi karibuni kwenye programu ya WhatsApp ya mfumo wa iOS, Kwa sasa bado toleo hili alijawafikia watumiaji hivyo hakikisha una sasisha (update) programu yako ya WhatsApp ya mfumo wa iOS kupitia App Store.