Programu ya WhatsApp Business au WhatsApp ya Biashara, imetengenezwa kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano kati ya watumiaji wa WhatsApp na wamiliki wa biashara ndogo ndogo. Programu hiyo ilizinduliwa rasmi mwezi wa tisa mwaka 2017 na kipindi hicho ilikuwa ni maalum kwa watumiaji wa mfumo wa Android.
Tokea mwaka 2017 hadi sasa ambapo ni takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa, sasa WhatsApp imetangaza kuleta programu hiyo kwa watumiaji wa iOS. Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya WhatsApp, programu hiyo imeanza kupatikana kuanzia siku ya jana kwa watumiaji wa iOS wa nchi za Brazili, Ujerumani, Indonesia, India, Mexico, Uingereza na Marekani.
Hata hivyo kupitia tovuti hiyo WhatsApp imeandika kuwa programu hiyo itawafikiwa watumiaji wote wa mfumo wa iOS kote duniani ndani ya wiki kadhaa zinazokuja. WhatsApp pia imetangaza kuwa watumiaji wote wa iOS pia watakuwa na uwezo wa kutumia programu mpya kwa ajili ya kompyuta ambayo inategemewa kuja sambamba na programu hiyo ya mfumo wa iOS.
Mbali na hayo kwa upande wa WhatsApp ya kawaida, hivi karibuni watumiaji wa programu hiyo wataweza kuzuia watu wasio wajua kuweza kuwaalika kwenye magroup bila ruhusa. Sehemu hiyo inategemea kuja hivi karibuni kwa watumiaji wote wa programu ya WhatsApp ya iOS na Android. Kujua zaidi kuhusu sehemu hii soma hapa.