Kama unavyojua unaweza kuhifadhi chat zako za WhatsApp kupitia sehemu mbalimbali, Kuhifadhi huku kunasaidia hata pale unapo poteza simu au kufuta programu ya WhatsApp kwenye simu yako basi utaweza kupata meseji zako zote ulizokuwa unatuma na kutumiwa kabla ya kupoteza simu yako au kabla ya kufuta programu ya WhatsApp.
Moja kati ya sehemu ambazo unaweza kuhifadhi (backup) data hizo ni pamoja na kwenye Google Drive. Sasa kama ni mara yako ya kwanza kusikia Google Drive, hii ni sehemu ya huduma zinazotolewa na Google na hii huja kama programu ambayo iko ndani ya simu zote za Android, kama vile inavyokuwa YouTube pamoja na Gmail.
Google Drive huja kwa wateja wote wa Google na hutoa kiasi cha GB 15 kwa ajili ya kuhifadhi data zako kupitia vifaa vyako vyote vinavyotumia huduma za Google. Google Drive inaweza kutumika kuhifadhi vitu kupitia kompyuta hata pia kwenye smartphone na hii huwa rahisi sababu vitu ulivyo hifadhi kwenye simu unaweza kuviona kwenye kompyuta na vitu ulivyo hifadhi kwenye kompyuta unaweza kuviona kwenye simu.
Kwa kuwa Google hutoa GB 15 pekee, hata pale unapofanya backup ya programu ya WhatsApp MB unazo tumia huesabiwa, yaani kama file lako lina MB 10 basi MB 10 upunguzwa kwenye zile GB 15 ambazo unapewa bure na Google.
Sasa hivi leo Google imetuma barua pepe kwa wateja wake wote ikiwajulisha kuwa hivi karibuni watumiaji wa programu ya WhatsApp wataweza kufurahia kuhifadhi data zao kupitia Google Drive bila data hizo kuhesabia kwenye zile GB 15 ambazo unapewa bure. Yaani sasa hata kama unafanya backup ya muda mrefu kiasi gani hata kama backup hiyo ina GB 10 basi GB hizo hazito hesabiwa kwenye zile GB 15 ambazo unapewa unapojiunga na huduma za Google ikiwa pamoja na Google Drive.
Hata hivyo Google imesema huduma hiyo inatarajiwa kuanza rasmi kwa wateja wote kuanzia November 12, 2018 na hii ni kutokana na makubaliano ambayo Google imeingia na WhatsApp kuweza kutoa huduma hiyo bure kabisa. Unaweza kuangalia barua pepe yako ya Gmail na utoana barua pepe yenye kichwa cha habari “Change to WhatsApp Backups in Google Drive“.
Sasa inawezekana hujui jinsi ya kufanya backup kupitia app ya WhatsApp kwenda kwenye Google Drive, Sasa kama hujui unaweza kufanya hatua hizi. Fungua programu ya WhatsApp, kisha bofya vitufe vitatu kwa juu kisha chagua Settings, alafu chagua Chats kisha shuka chini kidogo utaona sehemu iliyo andikwa Chat backup, kisha utaona sehemu imeandikwa Back up to Google Drive chagua muda unaotaka kufanya backup, au bofya Backup Now kuhifadhi data zako kwa muda huo.