Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Western Digital Yaleta Hard Disk za TB 14 na TB 12

Kwa mara nyingine kampuni nyingine imevunja rekodi ya hard disk kubwa kuliko zote duniani
Hard Disk Hard Disk

Kampuni maarufu ya teknolojia ya Western Digital, inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya data kama vile hard disk, flash drive na vifaa vingine kama hivyo hivi karibuni imetangaza sasa inafanya majaribio ya kuingiza sokoni hard disk zenye ukubwa wa Terabit 14 (TB14).

Ikiwa ni moja kati ya kampuni zilizojiwekea rekodi kwa kuleta hard disk hiyo ya TB 14, Western Digital kwa sasa inasambaza hard disk hizo kwa wateja maalumu kwaajili ya kufanyiwa majaribio ili ziweze kuingia sokoni mapema mwaka 2017.

Advertisement

Western Digital imeongeza ufanisi zaidi katika utengenezaji bidhaa bora za teknolojia baada ya kampuni hiyo kununua kampuni ya SanDisk, kampuni ambayo mwaka huu ilitoa memory card kubwa kuliko zote ya 1TB. Hata hivyo kampuni ya Western Digital bado haijatangaza hard disk hiyo itapatika kwa bei gani. Hard disk hii inategemea kutoka kwa matoleo mawili ambayo ni ya 14TB na 12TB.

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use