Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Utaweza kufunga sehemu ya SMS, Call logs na hata Instagram na Facebook
Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android) Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Wakati ikiwa bado haija fahamika kwa uhakika ni simu gani ya kwanza kuja na fingerprint, lakini ni wazi kuwa sehemu hii imekuwa ni sehemu ya muhim kwenye simu nyingi sana hasa kwa upande wa ulinzi.

Kuliona hili leo kupitia makala hii nimekuletea njia rahisi na ya haraka ambayo unaweza kutumia kuweka ulinzi wa fingerprint kwenye kila application unayotumia kwenye simu yao. Sehemu hii inafanya kazi kama ilivyo kwenye sehemu ya Fingerprint kwenye programu ya WhatsApp.

Advertisement

Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi moja kwa moja twende kwenye hatua kwa hatua jinsi ya kuwezesha ulinzi wa fingerprint kwenye app zako zote. Kitu cha muhimu kumbuka ni lazima simu yako iwe imewezeshwa na ulinzi huu, yaani ni lazima simu yako iwe na sehemu ya fingerprint.

Kama simu yako tayari inayo sehemu hiyo, basi moja kwa moja unaweza kuendelea kwa kufuata hatua hapo chini. Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini kisha install kwenye simu yako ya Android.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app moja kwa moja fungua app hii na moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa kutengeneza password.

Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Baada ya kutengeneza password na kurudia mara mbili bofya alama ya tiki iliyopo chini upande wa kulia. Baada ya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa kuweka ulinzi wa fingerprint kwenye app unayotaka. Bofya kitufe cha Jumlisha kuweka Apps.

Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Baada ya hapo moja kwa moja utaletewa list ya apps ambazo zipo kwenye simu yako na moja kwa moja chagua app unayotaka kuweka ulinzi wa fingerprint, bofya sehemu ya switch kuweka ulinzi kwenye app uliyoichagua.

Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Baada ya hapo bofya kitufe cha jumlisha kinachotokea upande wa kulia chini na moja kwa moja utapelekwa kwenye hatua inayofuata.

Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Baada ya hapo unatakiwa kuwezesha app hii kupitia permission mbalimbali, hakikisha unabofya sehemu ya OK ili kuweza kuwezesha app hii kwenye permission zote ili iweze kufanya kazi vizuri.

Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona apps zako zote ulizo chagua zina ulinzi wa fingerprint na kila wakati unapo fungua app yenye ulinzi unatakiwa kuweka alama ya fingerprint ili kuweza kufungua app hiyo.

Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Kama unavyoweza kuona hiyo ndio njia fupi ambayo unaweza kutumia kuweka fingerprint kwenye app yoyote kwenye simu yako ya Android. Kumbuka kama sehemu ya fingerprint haifanyi kazi vizuri basi unaweza kutumia password kwa kubofya alama ya keyboard iliyopo chini upande wa kulia.

Weka Ulinzi wa Fingerprint Kwenye App Yoyote (Android)

Hiyo ndio njia fupi ambayo unaweza kutumia kuweka ulinzi zaidi kwenye apps mbalimbali unazo tumia kwenye simu yako, kumbuka unaweza kuweka ulinzi huu sehemu yoyote kwenye simu yako. Kama haitoshi unaweza kuangalia hatua kwa hatua jinsi ya kuweka password kwenye sehemu yoyote kupitia simu yako ya Android.

Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku, pia usisahau kujiunga na channel yetu ambayo huwa tunajifunza mambo kwa vitendo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use