Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

WCB Wasafi Yaleta Tovuti ya Kuuza na Kununua Nyimbo Mtandaoni

Msanii diamond wa Tanzania sasa kuamua kuingia mtandaoni
Wasafi.com Wasafi.com

Msanii maarufu wa hapa Tanzania Diamond Platnumz kupitia kampuni yake ya WCB Wasafi hivi leo imetangaza kuwa sasa nyimbo zake zitapatikana kupitia mtandaoni kupitia tovuti mpya ya kampuni ya hiyo yenye jina la wasafi.com.

Akielezea ujio wa mtandao huo mpya wa wasafi.com, msanii diamond platnumz amesema kuwa mtandao huo sio kwaajili ya wasanii kutoka kampuni hiyo pekee, bali mtandao huo wa wasafi.com utakuwa kwaajili ya wasanii wote wa tanzania wanaotaka kuuza nyimbo zao nje na ndani ya Tanzania kupitia mtandao huo.

Advertisement

Tovuti hiyo ambayo kwa sasa tayari iko hewani ni rahisi sana kutumia na kama msanii huyo alivyo eleza huna haja ya kujisajili kwanza ndio ununue bali utaweza kununua mara moja, lakini pia kama ungependa kuwa na akaunti kupitia mtandao huo basi utaweza kuwa na akaunti yako ambayo utaweza kuweka pesa kwaajili ya kununua audio au video yoyote mpya itakayowekwa kwenye mtandao huo mpya wa wasafi.com.

Tovuti hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya Setup Ltd inaonekana kuwa na muonekano ambao ni mzuri na ambayo ni rahisi kutumia kwa kila mtu anaejua maswala ya mitandaoni na hata kwa wale ambao hawajui kabisa. Toviti hiyo pia ina vigezo na masharti ambavyo ni vizuri kusoma kwani katika swala la kununua nyimbo (hati miliki) ni vyema kujua masharti ya matumizi ya tovuti hiyo pamoja na kazi za wasanii zilizoko kwenye tovuti hiyo mpya ya wasafi.com.

Kujua zaidi kuhusu tovuti hiyo unaweza kutembelea Tovuti hiyo ya wasafi.com au angalia video hapo juu au unaweza kutembelea tovuti ya millardayo.com kupata habari kamili kuhusu tovuti hiyo.

[ratings]

9 comments
    1. Msomorohd Ndio nahisi zitakwepo kama ata kwenda kuzungumza na wenye mtandao, ni kama alivyosema mwenye mtandao huo.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use