Google ni moja kati ya kampuni nyingi zenye kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jamii, moja ya kati ya matokeo ya tafiti mpya kutoka Google ni app mpya ya Google Live Transcribe.
App hii mpya kutoka Google imetengenezwa kwa lengo kubwa la kusaidia watu wasio sikia vizuri, mbali na hayo app hii mpya inaweza kutumika kwa namna mbalimbali hata na watu wasio na matatizo ya kusikia.
App hii inauwezo mzuri wa kuweza kuandika maneno yote ambayo unayatamka kwa maandishi, App hii ya Google Live Transcribe ina uwezo wa kusikia zaidi ya lugha 70 huku lugha ya Kiswahili ikiwemo ndani yake. Unacho takiwa kufanya ni kudownload app hii kwenye simu yako ya Android kisha washa app hii kupitia sehemu ya accessibility kisha app hii itanza kutumia Mic ya simu yako kuweza kuandika maneno ambayo inayasikia.
Kitu cha muhimu unachotakiwa kukumbuka ni kuchagua Lugha unayotaka app hii iweze kusikia, kama unataka kusikia maneno ya kiswahili basi chagua Swahili, kama unataka kusikia english unaweza kuchagua english na app hii itanza kuandika maneno yote ya kingereza inayosikia.
App hii kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa Android, Unaweza kudownload app hii kupitia link hapo chini, pia usisahau kuwasha app hii kwenye sehemu ya accessibility. Pia kumbuka app hii inatumia Internet hivyo ni muhimu kuwa na internet kwenye simu yako ndipo app hii itafanya kazi inavyotakiwa.